Tuesday, February 22, 2011
KESI YA CHADEMA YAAIRISHWA MPAKA MACHI 25 HUKU MABOMU YAKIRINDIMA LEO TENA
Posted by woinde on Tuesday, February 22, 2011 in | Comments : 0
viongozi wa chadema wakiwa wanasikiliza kesi yao leo mahakamani
WAKILI upande wa Utetezi wa kesi inayowakabili wafuasi 30 wa Chama cha Chadema, Method Kimomogoro, ameiomba Mahakama kutokubaliana na ombi la upande wa Mashitaka, kuhusu kusogeza mbele shauri kwa madai upelelezi haujakamilika, kwani huo ni ujanja, na inaonyesha upelelezi umekamilika kutokana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuongelea kesi hiyo Bungeni.
Hayo aliyaeleza jana, Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Charles Magesa, wakati akijibu hoja iliyotolewa na Wakili upande wa Mashitaka, Wakili Msaidizi wa Serikali Haruna Matagane, ya kuomba kesi isogezwe mbele kwa kutokamilika kwa uchunguzi na kuwasilisha hati ya ofisi ya RCO ya kuomba kibari cha kusogeza mbele kesi.
Wakili Kimomogoro alisema kuwa, hakubaliani na ujanja unaofanywa na upande wa MaAshitaka, kwani hali halisi inaonyesha kesi hiyo uchunguzi wake umekamilika kwa sababu viongozi wa juu wa serikali kama Waziri Mkuu, ana ushahidi wote wa kesi na aliongelea kesi hiyo Bungeni ambapo nje ya Mahakama.
“Isitoshe pia tunasikia katika vyombo vya habari na kuona katika vyombo vya habari, Polisi wakitoa maelezo juu ya mwenendo mzima wa kesi hiyo, hivyo kwa haya yote inaonyesha kesi imekamilika, uchunguzi na inapaswa kusikilizwa” alisema Wakili Kimomogoro.
Alisema kuwa lazima ifike mahali Mahakama ichukulie kesi hiyo kwa uzito unaostahili na kuacha kusikiliza sababu za uongo za upande wa mashitaka, kwa sababu ziyo za kweli, ila zina nia ya kuchelewesha kesi.
Aidha aliiomba Mahakama hiyo, ipange tarehe ya mwisho ya kuahirisha kesi hiyo na isirudie tena kurusha tarehe, na tarehe ijayo isikilizwe kwa maelezo ya awali.
“Naomba piaa upande wa Mashitaka Mawakili husika wawakumbushe viongozi wa serikalini, kuacha kuingilia sula hilo la Mahakamani na kutoa matamko yanayoathri mwenendo wa kesi hii” alisisisitiza Kimomogoro.
Hata hivyo akijibu hoja hizo za Wakili wa upande wa Utetezi, Wakili upande wa Mashitaka, ambaye ni Wakili Msaidizi Upande wa serikali, Haruna Matagane, aliiambia Mahakama kuwa, kwa mujibu wa Jamuhuri, ndiyo inayohusika kuendesha kesi hiyo na hoja za kuwa Polisi wanatoa vielelezo vya kesi siyo za kuzisikiliza.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi siyo linaloendesha kesi hivyo hawahathiri kesi hiyo kwa jambo lolote, na kuomba mahakama hiyo ikubaliane na ombi lao la kutaka kesi isogezwe mbele kwa sababu uchunguzi haujakamilika.
“Mheshimiwa Hakimu, naomba shauri hili lisogezwe mbele kwa sababu hatujakamilisha uchunguzi wetu na pia tunaomba upokee hati ya ombi la kibari chaa kusogezwa mbele kesi hii, sababu uchunguzi unaendelea” alisema Matagane.
Naye Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Charles Magesa, akijibu hoja zilizotolewa Mahakamani hapo, alikubaliana na hoja ya Wakili wa Upande wa utetezi na kutoa onyo kwa wale wote wanaoeleza masuala ya Mahakamani nje ya Mahakama.
“Mahakama hii, inatoa onyo kuacha mara moja kwa mtu yoyote kuzungumzia kesi iliyopo Mahakamani, kwani wanaofanya hivi wanajuwa wazi sheria zinakataa na hata wale wanotoa vielelezo kwenye vyombo vya habari, nao waache mara moja, kwani wanavunja sheria inawakataza” alisema Magesa
Aidha Hakimu Magesa, alikubaliana na ombi la upande wa Mashitaka, lililotolewa na wakili Matagane, kuomba kesi isogezwe mbele, na kusema kuwa anakubaliana nayo kwa mujibu wa sheria na inakubalika kisheria.
Hakimu huyo pia alitoa hati ya kukamatwa kwa washitakiwa watano, ambao ni Elisante Noel, Peter Kimario, Mathias Valerian, Walter Mushi na Peter Maruwa, kwa kosa la kutofika Mahakamani hapo na hakuna maelezo yoyote ya kutofika Mahakamani hapo.
Hata hivyo kesi hiyo imehudhuriwa na washitakiwa 24, wakiwepo viongozi wote wa ngazi ya Taifa ya Chadema na wabunge, isipokuwa mbunge wa Jimbo la Rombo, Joseph Selathini hakuweza kufika Mahakamani hapo, kwa sababu ya matibabu anayopatiwa Hospitali ya Rufaa Muhimbili Dar Es Salaam.
Baada ya kumalizika kwa kesi hiyo, akizungumza nje ya Mahakama hiyo, mara baada ya kesi hiyo kuahirishwa, na umati mkubwa wa wananchi waliotinga Mahakamani hapo licha ya Polisi kutanda kona za Mahakama hiyo na magari yao, waliofika kusikiliza kesi hiyo, aliwashukuru kwa kufuatilia kesi hiyo na kuwataka wazidishe umoja huo katika kukomboa Taifa.
Alisema kuwa kwa Upande wa Chama hicho, kimeandaa maandamano ya nchi nzima, na yatakuwa ya MKoa kwa Mkoa na wataanza na Mkoa wa Jiji la Mwanza kesho, itafuatiw ana Mikoa mingine.
Alisema lengo kudaai haki za watanzania watatu waliopigw arisasi na Polisi Januari 5 mwaka huu, wakati wakidai haki yao ya msingi ya kumpinga Meya Haramu wa CCM, Gaudence Lyimo.
Naye Mbunge wa Arusha, Godbless Lema, akiwa anatembea kw amiguu na wafuasi wa Chadema, huku wakimshangilia kuwa “Waziri waziri, Waziri, Waziri” aliwaambia wafuasi hao kuwa wapo pamoja katika kudai haki nay eye anampinga sana Waziri Mkuu na ataendelea kumpinga mpaka kieleweke.
Hata hivyo baada ya Polisi kuona umaati wa watu ukishuka naa barabara ya Mahakamani, kabla ya kukamata barabara kubwa inayoungana na Uhuru, Polisi walifyatua mabomu matatu na kuwatawanyisha wafuasi hao mara moja na hali ikarudi kuwa shwari.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 25 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena na washitakiowa wote wako nje kwa dhamana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia