BREAKING NEWS

Wednesday, February 23, 2011

ARUSHA WAANDAA ARAMBEE YA KUCHANGIA WAATHIRIKA WA MABOMU GONGOLAMBOTO



MKOA wa Arusha umeanzisha utaratibu maalumu wa kukusanya na kuchangisha michango mbalimbali kwa ajili ya rambirambi kwa waathirika wa mabomu yaliyotokea Gongo la Mboto Februari 16 mwaka huu,jijini Dar esalaamu na kusababisha uharibifu mkubwa wa mali na watu 24 kupoteza maisha.



Mkuu wa mkoa wa Arusha,Isdori Shirima amewaambia waandishi wa habari ofisini kwake kuwa ,michango hiyo itakusanywa katika ofisi ya mkuu wa mkoa na amewataka wakazi mbalimbali wa mkoa wa Arusha,yakiwemo mashirika ya umma kutambua athari zilizowakumba wananchi wa eneo hilo ambao wengi wao wamepoteza mali nyinyi pamoja na viungo mbalimbali katika miili yao.



Adha kwa kutumia vyombo vya habari amewasihi wananchi kwa ujumla kuchangia mchango huo wa hiari,yakiwemo Mablanketi,Vitanda ,Mashuka,magodoro pamoja na fedha tasilimu zitakazosaidia waathirika hao wa mabomu kuweza kujinunulia mahitaji yao.



Alisema mkoa hauna budi kuungana na watanzania wenzetu kwa kutoa pole kwa ndugu ,jamaa na marafiki waliofikwa na janga hilo, hasa katika kipindi hiki kigumu ambapo taifa limepoteza nguvu kazi kutokana vifo vilivyotokea vya watu zaidi ya 20 waliotokana na kulipukiwa na mabomu hayo na kuharibu pia makazi yao ya kudumu.



Hata hivyo Shirima amewasihi wananchi waliopo karibu na maghala ya silaha ya kambi za jeshi, kuchukua tahadhali wakati kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa inasubili maelekezo ya serikali katika kujihami na hali hiyo isiweze kujirudia tena.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates