BREAKING NEWS

Friday, February 11, 2011

NYUMBA YA RUBANI YA GEUKA MATENGENEZO YA MAGARI YA WIZI

JESHI la polisi mkoani Arusha limekamata magari mawili ya wizi na watuhumiwa zaidi ya wanne wanashikiliwa,kwa kujihusisha na matukio ya uporaji wa magari hayo, ambapo wamekuwa wakibadili namba za usajili na rangi kabla ya kuyauza .



Kwa mujibu wa Kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha,Akili Mpwapwa , wakati akiongea na waandishi wahabari katika eneo la tukio hilo alisema kuwa magari hayo yamekutwa nyumbani kwa rubani wa ndege aliyefahamika kwa jina la ,James Nnko eneo la sombetini na kwamba mtoto wa Rubani huyo Isack James Nnko(31) ni miongoni mwa watuhumiwa waoshikiliwa kwa wizi huo wa magari.





Ambapo alisema kuwa motto wa rubani huyo ambaye ndiye anaishi katika nyumba hiyo inayomilikiwa na baba yake ambayo mali hizo za wizi zimekutwa huku zikiwa zinaendelea kubadilishwa rangi na baadhi ya vifaa vya ndani vya magari hayo.



Alisema kuwa mtuhumiwa mkuu ambaye ni mtoto wa rubani wa ndege Isack James Nnko awali kabla ya kuja hapa nchini alikuwa katika masomoni nchini Afrika kusini ambapo alirejea nchini siku za hivi karibuni.





Kamanda Mpwapwa alisema kuwa magari yaliyokamatwa na moja lililokuwa na namba za usajili T 170 AUL liliibiwa mnamo February 4 majira ya saa tatu usiku katika eneo la sakina ambalo ivi sasa limebadilishwa kadi na kukatiwa bima mpya huku likiwa na namba za usajili T 829 AZL ambalo lilikuwa limeshaanza kubadilishwa rangi na vifaa vya ndani.



Alisema kuwa gari lingine lilikuwa na namba za usaliji T225 ABC ambalo liliibiwa mnamo February 5 mwaka huu katika eneo la Motel 2000 ambalo nalo lilimeshabadilishwa namba za usajili na kuwa T316 BEE.



Alibainisha kuwa kuhusiana na tukio hilo wamekamatwa watuhumiwa zaidi ya wane akiwemo mtoto wa rubani Isack James Nnko .



Mmpwapwa aliongeza kuwa taarifa kuhusiana na tukio hilo katika nyumba hiyo walizipata kutoka kwa raia wema na amewaomba waendelee kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu pale zinapojitokeza na kutoa taarifa yoyote ambayo wanajua inafanywa kinyume cha sheria.





Aidha kamanda Mpwapwa amewasihi madereva taksi wanaofanya biashara ya kupakia abilia majira ya usiku mjini hapa kuhakikisha wanakuwa na zaidi ya mmoja kwenye gari ili kukabiliana na mataukio ya uhalifu.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates