Sunday, February 20, 2011
NMB YAKOPESHA VIKUNDI 353 VYA WAKULIMA WADOGO WADOGO
Posted by woinde on Sunday, February 20, 2011 in | Comments : 0
MKUU wa mkoa wa Arusha Isidore Shirima(katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa mkuu wa idara ya kilimo wa NMB ,Robert Paschal(kulia) wakati mkuu huyo, alipotembelea banda la NMB wakati akitembelea maonyesho ya bidhaa za wakulima wa kahawa na wanunuzi katika hotel ya Ngurdoto juzi,kushoto ni afisa uhusiano wa NMB nchini ,Shyrose Banji
BENKI ya NMB nchini imetumia zaidi ya shilingi bilioni 150 kukopesha vikundi 354 vya wakulima wadogo wa mazao ya biashara ikiwemo kahawa na korosho katika msimu wa kilimo.
Vikundi hivyo, ikiwa ni pamoja na wakulima wa kahawa wapatao vikundi 155 na wakulima wa korosho vikundi 199, vimekopeshwa kwa riba nafuu ,ikiwa ni utaratibu wa NMB kujikita katika kuwekeza kwenye sekta ya kilimo kwanza.
Akizungumza katika maonyesho ya kahawa ,katika mkutano wa wakulima na wanunuzi wa kahawa unaofanyika mjini Arusha,mkuu wa idara ya kilimo wa NMB ,Robert Paschal alisema ,benki hiyo imedhamilia kuwainua wakulima wadogo kwa kuwakopesha fedha kwa ajili ya kununua vitendea kazi ikiwemo mbolea na madawa,ikitumanini kuwa faida itakayopatikana kwenye mazao hayo itamsaidia mkulima kurejesha mkopo huo kwa kiwango nafuu.
''NMB itaendelea na utaratibu huo wa kuwakopesha wakulima baada ya kufanikiwa kwa muda mrefu wa kuwakopesha wakulima wa mazao ya biashara ya kahawa ,korosho ,ufuta ,ili mazao hayo yaweze kuzalishwa kwa vingi na kuapatia mazao ya kutosha''alisema
Nao wakulima wa kahawa,pamoja na kuipongeza NMB kwa mikopo inayoitoa mara kwa mara kwa wakulima wa mazao hayo ya baishara,wameishauri benki hiyo ijaribu kutoa mkopo kwa muda mrefu wa miaka mitatu ,tofauti na sasa ambapo hutoa mkopo kwa kipindi cha januari na desembe pekee.
Fatima faraji ni mkulima mdogo wa kahawa ambaye anatarajia kuchukua mkopo NMB kwa ajii ya kuendeleza kilimo cha kahawa ,alisema kuwa kwa pamoja na mkopo huo kuwanufaisha wakulima wenzake amedai kuwa muda wa marejesho uimekuwa ni mfupi na kujikuta wakulima wakishindwa kunufaika na kujikuta wakilipa benki pekee.
''mimi kama mkulima mrefu naiomba NMB na tasisi zingine za fedha zinazotoa mkopo kwa wakulima kuangalia namna ya kuongeza muda wa mkopo kwa wakulima ili fedha hizo zi weze kuwanufaisha ‘’alisema
Pamoja na kuipongeza NMB kwa kutoa mikopo kwa wakulima wadogo, Fajari ameishauri iangalie utaratibu wa kutoa elimu kwa wakulima wadogo ,kwani wengi wao wamekuwa hawana uelewa zaidi wa kilimo
Kwa upande wa wakulima wa kahawa nchini wameiomba serikali na asasi za fedha nchini kuwapatia mikopo ya muda mrefu ili waweze kuboresha kilimo chenye tija sanjari na kuongeza uzalishaji .
Nae Amir Hamza,ambaye ni mkulima na mnunuzi wa kahawa mkoa wa Kagera alisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili wakulima ni pamoja na uhaba wa vitendea kazi, hivyo ameishauri NMB kuangalina uwezekano wa kuwakopesha vitendea kazi ukiachiliambali fedha wanazotoa kwa mkupuo.
‘’unajua wakulima wengi hapa nchini hawatumii mbolea,ndio maana mazao ya kahawa yanakuwa sio mengi tofauti wa wenzetu wa nchi ya Vietinam ambapo mkulima anapolima heka moja atakuwa na uhakika wa kuvuna tani tatu ,kwa hapa Tanzania kilimo cha ekeri moja ya kahawa imekuwa haifikishi hata kilogram 800 ’’alisema na kuitaka NMB kutoa elimu pia kwa wakulima juu ya matumizi ya mikopo hiyo
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia