KAMPUNI ya uwakala wa kukusanywa ushuru wa maegesho ya magari mjini hapa,ya Kilimanjaro Millenium Printers Ltd(KMPL) ya mjini Arusha, imekusudia kuifikisha mahakamani kampuni ya kusafirisha watalii ya Rainbow ya mji hapa, kwa kukwepa na kugoma kulipa ushuru wa maegesho ya mageri yake kwa muda mrefu .
Mkurugenzi wa KMPL,Thomas Munis amesema kuwa,kampuni ya Rainbow imekuwa ikikaidi kulipa ushuru wa maegesho kwa muda mrefu na kusababisha ufumbufu mkubwa ,kwa wakala huyo kushindwa kufikia malengo ya kukusanya ushuru wa mapato ya serikali.
‘’kwa sasa tunawasiliana na wanasheria wetu ama wa manispaa ili kuifikisha mahakamani kampuni hiyo kwa akuendelea kutoa usumbufu mkubwa na kushindwa kulipa ushuru wamaegesho ya magari kinyume cha sheria’’alisema Munisi
Munisi,alisema kuwa licha ya kampuni yake kuandika barua za mara kwa mara kuikumbushia kampuni hiyo kulipa deni la zaidi ya shilingi 300,000 kwa kila gari,imekuwa ikizitia barua hizo kapuni hizo bila kuchukua hatua madhubuti.
Alisema hata barua ya mwisho ya tarehe 23/12 mwaka jana iliyoandikwa na mkurugenzi wa manispaa ya kuitaka kampuni hiyo iwe imelipa madeni ya maegesho ndani ya siku saba ,kampuni hiyo iliendelea kukaidi.
Alisema,kampuni hiyo iliendelea kukaa kimya ,hali iliyoilazimu kampuni yake iliyopewa dhamana ya kukusanya ushuru wa maegesho kisheria,juzi januari 4 mwaka huu kufika katika eneo la maegesho ya magari ya kampuni hiyo lililopo katika hotel ya Meza Lunna kijenge na kufunga kizuizi moja ya gari la kampuni hiyo lenye namba T 103 ABC aina ya Coaste.
Gari hilo lilikuwa limepakia watalii 6 wa kigeni na kusababisha adha kubwa kwa watalii hao raia wa nchini Uingereza na ufaransa ,kuachwa na ndege waliotajaria kupelekwa njini Nairobi kupakia ndege ya kuelekea nchini kwao.
Akizungumzia barua ya tarehe 23/12/2010 iliyoandikwa kwa kampuni hiyo ya Rainbow na Paul Mugisha ,kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa ya Arusha,ambayo nakala yake tunayo,aliitaka kampuni hiyo ya Rainbow kulipa deni la maegesho ndani yasiku 7,sehemu ya barua hiyo ilisomeka kuwa
‘’unatakiwa kulipa ushuru wa maegesho ya magari yako kuanzia tarehe 1/8/2010 kwa kampuni ya Kilimanjaro millennium Printers Ltd ndani ya siku saba kuanzia tarehe ya barua hii.
Barua hiyo iliendelea kusema kuwa’’usipotekeleza agizo hilo ndani ya siku saba kuanzia leo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yako na kampuni yako ikiwa ni pamoja na kuyakamata magari husika ,kutoza faini na riba ,kufuta matumizi ya eneo husika unaloegesha na kukuchukulia hatua zingine za kisheria’’
Nae mkurugenzi wa kampuni hiyo ya Rainbow ,Methew Mollel pamoja na kukiri kudaiwa na kampuni ya uwakala wa kukusanya ushuru(KMPL)hata hivyo alidai kudhalilishwa na wafanyakazi wa kampuni hiyo baada ya kufunga mnyororo gari yake iliyokuwa ikisafirisha watalii kwenda Nairobi kupanda ndege.
‘’ni kweli wanatudai lakini tangu walete barua yao ya kujitambulisha kuwa wamepewa jukumu la kukusanya ushuru wa maegesho ,hawakuwa wakifika kuchukua fedha zaidi ya kuona wanatuandikia barua wakitutaka tulipe fedha hata kwa mageri ambyo yamekuwa hayashindi hapo’’alisema na kuongeza kuwa
‘’wageni wetu wamedhalilishwa sana wamezuia gari yetu tangu saa 4 asubuhi hadi saa 8 mchana baada ya kuja askari polisi na kuwakamata vijana walihusika,hivi sasa ni saa kumi jioni wageni walitakiwa waondoke na ndege ya saa 8 mchana katika uwanja wa ndege wa kenyetta , hii gharama ya kuwalaza Nairobi nani ataipa,wametufanyia uhuni wa hali ya juu sana’’
Alisema kuwa kutokana na kadhia hiyo watalii hao waligoma kuondoka hali iliyolazimu kufika katika kituo cha polisi cha mjini kati kwa ajili ya kutoaa maelezo juu ya hatima yao huku wakitaka kulipwa fidia iwapo watakosa ndege Mjini Nairobi ya kusafiri kwenda kwao nchini Uingereza na ufaransa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa,Akili Mpwapwa alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo alisema kuwa baada ya kupata maelezo ya pande zote mbili wanajaribu kupitia mikataba ya kisheria ya kampuni hiyo ya uwakala wa kukusanya ushuru ili kujiridhisha.
’’kwa sasa tunapitia mikataba ikiwemo kuwakutanisha wahusika wote wawili na tutatoa ufafanuzi kwa kuwa tayari jalada la malalamiko limefunguliwa kwetu’’alisema
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
upo juu dada
ReplyDelete