KAMANDA wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenyi alizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kitendo cha wao kuzuia mkutano huu wa Chadema na alisema kuwa kuna vigezo viwili ambavyo vilisababisha wao kuzuia mkutano huo.
Sababu ya kwanza alisema kuwa ni kuwa chama hichi kimepeleka barua lakini hakija ainisha nia haswa ya kufanya mkutano huu pia chama hichi hakija timiza sheria ya kutoa barua kwani walitakiwa wakae masaa 48 lakini wao walikaa masaa 29 tu na walitaka kufanya mkutano mbali na hilo alisema kuwa kunataarifa pia wamepata kuwa iwapo mkutano huo ungefanyika basi kuna vijana ambao walikuwa wamejiandaa kwaajili ya kuiba maduka ya watu hizo ndizo sababu ambazo aliwaambia waandishi wa habari.
Kwa upande wa mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema yeye alisema kuwa walitimiza sheria zote na vigezo na pia alibainisha kuwa yeye alipoongea na kamanda wa polisi alisema kuwa amemwambia hana askari wa kutosha wa kuweza kulinda mkutano wake kwa iyo asubiri tena mpaka mwakani.
pia alibainisha kuwa mkutano huu ulikuwa sio wa kuvuruga amani bali na wakuongea na wananchi wake na pia alitaka kutumia mkutano huu kuwaeleza wananchi vitu ambavyo vinaendelea katika halmashauri ambazo chadema ndio wameshinda .
kwa upande wa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Mboye yeye alisema kuwa wamekubali kuhairisha mkutano huo kwa jana kwani walipigiwa simu na mkuu wa polisi said Mwema pamoja na msajili mkuu wa nyama wakiwataka waache kufanya mkutano huo na wasubiri wakae mezani wajadiliane.
Mbowe alisema kuwa wamekubali lakini wanawapa mpaka tarehe nne mwakani wawe wamewaita na wamekubaliana lasivyo tarehe tano wataenda kufanya mkutano na huo utakuw ani mkutano wa kudai akizao na watatumia nguvu ya uma na kuwaeleza wananchi ambao wamewatuma kila kitu ambacho wanafanyiwa ikiwa ni pamoja na uzalilishaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya viongozi wa serekali ambao wanajua sheria lakini wanazitegua.
Pia aliitaka serekali hususa ni waziri wa tami semi kumchukulia sheria kali mkurugenzi wa halmashuri ya Arusha pamoja na Ocd wa wilaya ya Arusha kwani alisema kuwa ndio wanachingia kwa kiasi kikubwa kuvuruga amani katika jiji la Arusha.