SOKWE MTU WA MAHALE AKIWA KATIKA POZI




SERIKALI kwa kushirikiana na shirika la hifadhi ya taifa (TANAPA) ipo katika mchakato wa mwisho wa kukipandisha hadhi kisiwa tarajiwa cha Saa nane kilichopo katika mkoa wa Mwanza kuwa hifadhi ya taifa

Rai hiyo ilitolwewa na kaimu mkurugenzi mkuu wa kisiwa hicho Donats Kayona wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea kisiwa hicho ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo katika visiwa hivyo

Kwa mujibu wa Kayona alisema kuwa tafiti mbalimbali zimeshafanyika ili kuweza kubaini ni wanyama wa aina gani ambao wataaweza kuishi katika kisiwa hicho kwa kuzingatia mahitaji ya kiikolojia

“Wataalamu kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam wameshafika katika kisiwa hiki na kufanya utafiti wa hali ya juu wa wanyama ambao wataweza kuishi katika kisiwa hiki ili kuongeza vivutio vya utalii katika kisiwa hiki na kwamba serikali ipo kati mchakato wa mwisho kabisa wa kukipandisha hadhi kisiwa hiki kuwa hifadhi ya taifa” alisema Kayona

Kayomba alisema kwa sasa kisiwa hicho kina vivutio mbalimbali vya utalii kama vile mapango makubwa ya kuvutia yaliyozingirwa na miamba Swala, Mijusi ya aina mbalimbali,Kobe,Paka Mwitu, Nyoka Mamba aina na aina mbalimbali za ndege

Aliwataja wanyama watakaoongezwa mara baada ya kisiwa hicho kuwa hifadhi ya taifa ni pamoja na pundamilia,mbuzi mawe,Swala granti Dikidiki,Kobe na kwamba itachangia kwa kiasi kikubwa kukidhi mahitaji ya watalii wa ndani na nje

Mbali na mafanikio hayo Kayomba alisema kuwa kisiwa hicho kinakabiliwa na changamaoto kadha wa kadha ikiwemo miundo mbinu ya uendeshaji pamoja na usafiri kwani kisiwa hicho kina boto ndgo na kwamba watalii hupendela boti kubwa

“Tunakabiliwa na changamoto ya usafiri katika kisiwa hiki kwani watalii wengi hawpendi kutumia boti ndogo jambo mablo limekuwa likichangia kwa kiasi kikubwa kutopata wageni wakutosha kwa kuzingatia kuwa hii ni hifadhi pekee hapa nchini kati ya hifadhi 15 iliyopo ndani ya maispaa ya mji wa Mwanza

Kisiwa tarajiwa cha Saa nane kina ukubwa wa kilimita 0.7 za mraba na kwamba miaka 1964 kilikuwa pori la akiba na ilipofika mwaka 2008 kilikabidhiwa rasmi katika shirika la hifadhi ya wanyama pori(TANAPA)

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post