WAZIRI wa viwanda,biashara na masoko nchini,Cyril Chami jana alianza “kutema cheche”mara baada ya kuwaambia watumishi wa idara mbalimbali katika wizara hiyo ya kuwa hatakuwa na msalie mtume kwa mtumishi yoyote ambaye ataonekana kulegalega katika utendaji wake wa kazi pamoja na wale wanaoendekeza tabia ya uvivu.
Alitoa karipio kali kwa watumishi wa wizara hiyo hususani wale wenye tabia ya kufarakanisha,wavivu pamoja na wale ambao huendekeza majungu na kuwatamkia ya kuwa ni vyema wakapisha mapema kabla ya kusubiri kuondolewa ama kufukuzwa.
“Kwa kweli wale watumishi ambao ni kikwazo cha maendeleo ndani ya wizara yetu,wenye kufarakanisha watu,wavivu na wanaopenda majungu huu sio muda wao naomnba watupishe sisi tufanye kazi”alisema Chami
Chami,alitoa angalizo hilo mara baada ya kufanya ziara ya siku moja jana jijini Arusha ambapo alitembelea taasisi ya utafiti wa kiinjia na maendeleo(TEMDO),Kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini(Camartec) sanjari na shirika la kuhudumia viwanda vodovidogo(SIDO) mkoani Arusha.
Akizungumza na wafanyakazi wa taasisi ya Utafiti wa Kiinjinia na Maendeleo(TEMDO) waziri Chami alitema cheche kwa kuwaambia ya kuwa watumishi hao hawana budi kucha tabia ya uvivu ikiwa ni pamoja na kuwa wabinifu katika shughuli zao mbalimbali.
Hatahivyo,aliuambia uongozi wa taasisi hiyo ya kuwa sasa ni muda wa wao kutangaza bidhaa zao ili kumudu soko la ushindani duniani kote huku akitoa ahadi ya serikali kuisadia taasisi hiyo kutangaza bidhaa zake.
Awali akitembelea kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini(Camartec), waziri huyo alishuhudia matrekta mbalimbali yanayotengenezwa katika kituo hicho huku akkiupongeza uongozi wa kituo hicho kwa kubuni mradi wa gesi ya kinyesi cha binadamu .
Waziri Chami alihitimisha ziara yake kwa kutembelea shirika la kuhudumia viwanda vidovidogo nchini(SIDO) mkoani Arusha ambapo alipata fursa ya kuzungumza na watumishi wa idara hiyo sanjari na uongozi wake ambapo alitoa pongezi kwa shirika hilo kwa kutoa mikopo mbalimbali kwa wajasiriamali wadogowadogo.
Naye mkurugenzi wa shirika hilo mkoani Arusha,Isdori Kayenze alimwambia wziri huyo ya kuwa pamoja na changamoto lukuki wanazokabiliana nazo lakini uongozi wake umefanikiwa kutoa jumla ya mikopo 156 kwa wajasiriamali wadowadogo mkoani hapa yenye gharama ya sh,280,512 milioni kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka jana.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia