mwakilishi wa NMB kanda ya kaskazini ,Feruzi Korongo (kushoto) akimkabidhi vifaa vya michezo kaimu katibu tawala wa mkoa,Jackson Sitabau katika jengo la ofisi ya mkuu
Benk ya NMB kanda ya kaskazini ,imekabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu ya mkoa ya Netibol (CHANEA)kwa ajili ya mashindano ya kuunda timu ya Taifa (TAIFA CAP)yanayotarajiwa kutimua vumbi desemba 16 mwaka huu, Kibaha mkoani Pwani.
Vifaa hivyo ambavyo ni ,Jezi,bukta,Soks, Flana,na Traksuti vilikabidhiwa katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha,kufuatia maombi maalumu yaliyotolewa na uongozi wa timu hiyo ikiwa ni sehemu ya kufanikisha mpango wa mashindano hayo kwa timu hiyo .
Akikabidhi msaada huo ,kwa kaimu katibu tawala wa mkoa ,Jackson Saitabau ,mwakilishi wa NMB kanda ya kaskazini,Feruzi Korongo ,alisema kuwa ,NMB imetoa msaada huo kwa kutambua na kuthamini umuhimu wa michezo nchini,na kwamba itaendelea kusaidia sekta hiyo ili kuboresha michezo nchini kwa kutenga sehemu ya faida inayoipata.
''NMB inaamini kwamba ili kupata wachezaji wazuri wa ngazi ya taifa ni lazima waanze kuandaliwa kwa ubora toka ngazi ya chini watakao iwakilisha taifa vyema kwenye michuano mbalimbali''alisema Korongo
Aidha aliwaasa wachezaji hao kujituma kwa nguvu zao zote kuhakikisha wanalete ushindi utakaoleta heshima kwa mkoa na kwa wale wote waliojitolea kusaidia kwa hali na mali.
Kwa upande wa kaimu katibu Tawala ,pamoja na kuishukuru NMB kwa kuthamini na kuchangia michezo ,ameiomba benki hiyo kuendelea kutoa msaada , kadri inavyo pata faida ,na alitumia fulsa hiyo kuwahimiza wachezaji hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu wawapo katika mashindani hayo.
‘’michezo kwa sasa ni ajira kwa hiyo nawaombeni mkajitume muweze kuuletea heshima mkoa ,na mtambue kuwa mkicheza vizuri mtapata ajira na kuwa mabalozi wazuri sehemu muendako,alisema Saitabau
Saitabau aliyataka mabenki mengine , taasisi za fedha na wadau wa michezo nchini kuiga mfano wa NMB katika kutambua umuhimu wa kuchangia michezo ili kujenga na kuimarisha afya za wachezaji hao sanjari na kupata wachezaji bora na wenye vipaji watakao weza kuliwakailisha taifa katika michezo mbalimbali.
Aidha aliwataka wafanyakazi maofisini kujenga utaratibu wa kushiriki michezo mbalimbali ,kwani hali hiyo itasaidia kujenga afya zao na kupunguza magonjwa ya ajabu ajabu yanayowanyemelea baadhi ya wafanyakazi ambao wengi wao wamekuwa wakinenepeana kwa kula vyakula ovyo ,hali ambayo imekuwa ikiwasababishia kuugua kila mara .
Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza desemba 16 hadi desemba 23 mwaka huu ,mjini Kibaha ,yanashirikisha timu zote za Netibol kutoka mikoa yote ya bara na viziwani ,ambapo yanalengo la kuunda timu moja ya Taifa(TAIFA QEENS) itakayoshiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa