BREAKING NEWS

Wednesday, December 29, 2010

MANYARA WAWASILISHA MIPANGO INAYOUNDA MAENDELEO



Ofisa mipango wa mji mdogo wa Mirerani,Raphael Mawi akisoma makadirio ya bajeti ya mji huo kwa mwaka 2011-2012 kwenye kikao kilichofanyika



MAMLAKA ya mji mdogo wa Mirerani,wilaya ya Simanjiro,mkoani Manyara imewasilisha mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa kata mbili zinazounda mamlaka hiyo.

Katika mapendekezo hayo bajeti ya maendeleo ya mwaka 2011-2012 ya mji mdogo wa Mirerani iliyokadiriwa kutumia kiasi cha sh2 Bilioni ilipitishwa na wajumbe wake.

Ofisa mipango wa mji huo,Raphael Mawi,akisoma makadirio ya bajeti hiyo juzi,kwa niaba ya Ofisa Mtendaji wa mji huo,Albert Ngala alisema mgawanyiko wake umejikita kwenye miradi ya maji,elimu,barabara na mengineyo.

Mawi alisema kwenye ujenzi wamepanga kutumia sh 1.36 Bilioni katika kutengeneza barabara za mitaa ya mji ambazo ziliharibika kutokana na mvua za el nino na fedha hizo waliahidiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa.

Alisema kwenye kilimo na mifugo wamepanga kutumia sh 86 milioni za uendeshaji mfereji wa shango,josho la mifugo,mbouti,banda la machinjio ya mbuzi,kuingiza umeme na maji machinjioni na nyumba ya mtumishi.

"Tutatumia sh80 milioni kwenye mradi wa maji katika mitaa ya Songambele B na Sokoni,Songambele A na Mirerani pamoja na ujenzi wa tanki la maji," alisema Mawi.

Kwenye elimu alisema watatumia sh41 milioni kujenga madarasa matatu ya shule ya msingi Zaire na kujenga nyumba ya walimu wa shule ya sekondari Mirerani Mkapa.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates