WAANDISHI WAKIWA NJE YA LANGO LA HIFADHI YA GOMBE LILOSHEHENI MNYAMA AINA YA SOKWE MTU





Serekali imetakiwa kusaidia kukuza utalii ulioko katika hifadhi za taifa zilizoko katika ukanda waMagharibi, mikoa ya Mwanza, Kigoma na Rukwa kwa kuwashirikisha mabalozi wa Tanzania waliko katika nchi Burundi na kongo .



Hayo yameelezwa na muhifadhi mkuu wa hifadhi ya Gombe iliyopo ndani ya ziwa Tanganyika mkoani Kigoma Noelia Myonga wakati akiongea na waandishi wa habari waliotembelea katika hifadhi hiyo.



Alisema kuwa iwapo serekali ita shirikiana na Tanapa kuunganisha balozi mbalimbali za nchi itasaidia kukuza utalii hapa nchini.



Alibainisa kuwa katika miaka ya nyuma utalii uliokuwepo juu kabla ya kuvunjika kwa amani kwa nchi za jirani ikiwemo Kongo na Burundi .



‘’nasema hivyo kwa kuwa ukiangalia utalii uliopo katika nchi hizi unakaribia kufanana na wanchini kwetu kwani ukiangalia katika nchi hizi kuna wanyama ambao nao pia wapo huku ukiangalia mnyama aina ya Sokwe na Gorila kwani wanyama hawa pia wanapatikana katika nchi hizi’’alisema Mnyonga.



Alifafanua kuwa pia serekali inatakiwa kuchukua hatua za makusudi za kuhifadhi maeneo yaliyosalia ya makazi ya sokwe wapatao 1870 walioko nje ya mipaka ya hifadhi .



Aliongeza kuwa sokwe ni mnayama adimu sana anayepatikana katika baadhi ya mbuga zilizopo hapa nchini hivyo serekali inatakiwa kujitaidi kushirikiana nao ili kuweza kuwalinda sokwe hawa waliobaki ambao ni vivutio sana kwa watalii wa ndani na wanje kwani tabia zake n maumbile yake yanakaribiana na binadamu wa kawaida.



Mnyonga alisema kuwa anapenda kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kutembelea mbuga zao ili kujionea vivutio vilivyopo katika mbuga izo ambazo zinavutia wangeni mbalimbai kutoka nje ya nchi.

Katika hifadhi hii ya Gombe kuna vivutio vingi ikiwemo wanyama pori mbalimbali kama vile sokwe mtu ,pia kuna maporomoko ya maji ambayo yanavutia mbali na maporomoko kuna samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika ziwa Tanganyika pamoja na michezo ya maji ya aina tofauti tofauti.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post