BREAKING NEWS

Friday, December 17, 2010

Watanzania wametakiwa kujijengea desturi ya kutembelea mbuga za wanyama zilizopo hapa nchini ili kujionea vivutio vilivyopo na sio kuwaachia wageni wanaotoka nje .



Changamoto hiyo ilitolewa na muhifadhi mkuu wa kisiwa cha Lubondo kilichopo ndani ya ziwa Victoria Batiho Herman wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliotembelea kisiwa hicho ikiwa ni moja ya safari yao ya ziara ya kutembelea na kujionea vivutio mbalimbali vilivyopo katika mbunga za wanyama hapa nchini.

‘Ufike wakati sasa kwa watanzania kuachana na mawazo mgando ya kuwa mbunga za wanyama zinatembelewa na watalii kutoka nje ya nchi tuu na waelewe kuwa hata wao ni watalii na wanatakiwa kujionea vivutio vilivyopo katika mbuga zetu”alisema Batiho

Kwa mujibu wa Batiho aliongeza kuwa ni wajibu wa kila mtanzania kujua vivutio hivyo kwa kujijengea tabia ya kutembelea mbuga zetu kwa kadri wawezavyo na kusisitiza kuwa watumie muda wao wa mapumziko kutembelea mbuga hizo.

Alibainisha mbali na mbuga hizi kuwa hapa nchini bado idadi ya watalii wanaotoka ndani ya nchi ndogo ikilinganishwa na ile ya watalii wanje na kwamba takwimu za kisiwa kisiwa hi twakimu za kisiwa hicho zinonyesha kwa mwaka 2009/2010 watalii wanje walikuwa 350 hukuwatalii wa ndani ambao ni watanzania wakiwa ni 277.



Aliendelea kufafanua kuwa kwa mwaka 2010/2011 kuanza Januari - Novemba watalii kutoka nje ya nchi walikuwa 243 na kwmba watalii wa ndani (wazawa) walikuwa 231 jambo linalodhihirisha kuwa umako wa watnzania kutembela mbunga za wanyama zilizopo hapa nchini bado ni mdogo



Kisiwa cha Rubondo kina vivutio mbalilmbali kama vile mnyama aina ya Statunga ambaye hakuna hifadhi hapa nchini ambayo ina mnyama wa aina hiyo lakini mbali na hilo kuna kisiwa cha ndege ambacho kuna zaidi ya aina 200 za ndege.



kisiwa hicho kina jumla ya visiwa vidogovidogo kumi na moja ambapo alivitaja kuwa ni Chitebe,Rubiso,itomi,Mizo,Kalera,Eroba,Chambuzi,Manyila ,Makozi,Izilambuba pamoja na Kageye .
















Baadhi ya waandishi wa habari wakipata msosi mara baada ya kutoka katika hifadhi ya Lubondo katika mgahawa ujulikanao kama kwa mama Nasoro uliopo nje kidogo wa mji wa Mwanza katika msafara huu mpiganaji Mussa Juma ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikosi hichi au kwa luga ingine msafara huu

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates