BREAKING NEWS

Friday, June 10, 2011

AFARIKI DUNIA NA MUNGINE KUKATWA MIGUU YOTE

Mtu mmoja amefariki dunia na mungine kujeruliwa vibaya baada ya pikipiki ambayo alikuwa anaendesha kukongana na gari uso kwa uso.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Akili Mpwapwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea jana June tisa mwaka huu majira ya saa 1:30 asubuhi katika barabara ya sakina manispaa ya jiji la Arusha kwenye barabara ya Nairobi mkoani hapa .

Alisema kuwa siku ya tukio hilo pikipiki yenye namba za usajili T154 BQW aina ya Toyo iliyokuwa ikitokea Ngaramtoni kuelekea mjini iliyokuwa ikiendeshwa na Lobulu Losanyika (18)muarusha makazi wa Kilimeru olasiva wilayani Arumeru aligongana na gari yenye namba za usajili T701 AJJ Toyota land cruser iliyokuwa ikiedeshwa na Ander Mattson(67) raiya wa nchini sweeden ambaye ni mkazi wa njiro na kusababisha kifo cha dereva wa pikipiki papo hapo.


Aidha alibainisha kuwa dereva piki piki alikuwa amepakiza abiria katika piki piki yake aliyejulikana kwa jina la Michael Thobias (16)muarusha na mkazi wa Olasiva ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari ya mringa iliyopo Ngaramtoni ambapo abiria huyo amevunjika miguu yote miwili .

"chanzo cha ajali hii ni kwamba mwendesha pikipiki alikuwa anakwepa gari aina ya prado iliyokuwa upande wake na kuingia upande wa pili ambapo alipoingia alikutana na gari hilo aina ya land cruser lilikuwa linatokea mjini kuelekea ngaramtoni uso kwa uso akashindwa kuikwepa na kusababisha ajali hiyo kutokea ambapo ilisababisha kifo hicho cha dereva papo hapo'alisema Mpwapwa.

Aidha alisema kuwa polisi walipofika hapo walimchukuwa majeruhi huyo na kumkimbiza katika hospitali ya mkoa ya Mounti meru kwa matibabu lakini baadae majeruhi huyo alihamishiwa katika hospitali ya seliani kwa matababu zaidi huku mwili wa marehemu ukiwa umeifadhi katika chumba cha kuifadhia maiti cha hospitali ya mkoa.

Ametoa wito kwa madereva pikipiki kufata sheria za usalama wa barabarani ili kuweza kupunguza ajali za pikipiki ambazo zimekuwa zikitokea mara kwa mara mkoani hapa.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates