BREAKING NEWS

Tuesday, June 21, 2011

HANIFA AANDAA ONYESHO LA MAVAZI ARUSHA

mwanamitindo wa mavazi maarufu hapa nchini,Hanifa Hashi akishirikiana na hoteli ya kitalii yenye hadhi ya nyota nne Mt,Meru wamepanga kufanya onyesho kubwa la mavazi litakalofanyika mapema katikati ya mwezi Okotoba mwaka huu.



Hayo yalisemwa na afisa mahusiano wa hoteli hiyo,Mariki Theron wakati wa onyesho la mavazi lililofanyika hivi karibuni na kudhaminiwa na hoteli hiyo onyesho lililolenga kusaidia kundi la jamii ya Albino waishio mkoani Arusha.



Mariki,alisema kuwa mara baada ya uongozi wa hoteli hiyo kutambua jitihada zinazofanywa na mwanamotindo Hashi katika kusaidia makundi mbalimbali yasiyojiweza ndani ya jamii kupitia mitindo wao walifarijika na kuamua kumuunga mkono mwanamitindo huyo.



Naye mwanamitindo Hashi ambaye amefanya kazi yake kwa miaka minane sasa alisema kuwa mara nyingi amekuwa akifanya maonyesho kwa lengo la kusaidia jamii huku akibanisha kuwa mbali na kusadia kundi la jamii ya Alibino waishio mkoani Arusha pia amesaidia vikundi vya Maridadi na kituo cha yatima cha Moshi-Arusha kupitia fani yake.



“Lengo langu ni kusaidia makundi yasiyojiweza ndani ya jamii kwa kuwahamasisha lakini vilevile nashukuru kwani kupitia fani hii nimeweza kusaidia watoto 21 kwa kuwapatia makazi katika eneo la Makao Mapya hapa Arusha”alisema Hashi

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates