BREAKING NEWS

Monday, June 6, 2011

PROFESA AGUNDUA DAWA YA UKIMWI ARUSHA



profesa Laizer akiwa anawagaiwa watu waliofika kwake dawa kwa ajili ya magonjwa mbalimbali yanayowasumbua



Profesa Laizer akiwa na msaidizi wake Elias lendima wakiwa wanataarisha dawa hiyo kwaajili ya kuipika.



miti inayochemshw ili kutengeneza dawa

akiandaa dawa ipo jiko
Dawa ya kutibu magonjwa sugu ijulikanayo kwa jina la kitaalamu Casissaedulis/sprinorum kwa jina la kimasai Olamuriki ambayo yanatatiza dunia iliyotafitiwa kitaalamu tayari imegundulika na inasemekana mpaka sasa imeshatibu watu wengi ambao walikuwa wanaumwa magonjwa mbalimbali ikiwemo gonjwa hatari la ukimwi.

Dawa hiyo ambayo ambayo yenyewe inanyweka na inatumiwa kulingana na ugonjwa wa mtu pamoja na dozi kufuatia majibu ya daktari ambayo mgojwa amepewa ni tofauti na nyingine amb azo watu mbalimbali wamekuwa wakizitoa na kudai kuwa wameoteshwa huku wengine wakisema kuwa wametokewa na mizimu ya kale.

Profesa Japhat Kimenenga Laizer ambaye ni mtafiti pekee kwa Tanzania kugundua dawa hiyo ya kutibu magonjwa haya sugu kama ukimwi ,Kansa namengineyo mengi ambaye k alizungumza na kudai kuwa amefanya utafiti kwa muda mrefu na amebainisha kuwa alianza kufanya utafiti huo tangu mwaka 1984 huku akiawa ameanza kutoa dawa kwa wagonjwa tangu mwaka 2006 huko katika kijiji chake cha Ng'aritati kilichopo katika kata ya Makiwaro wilayani Siha ambapo amebainisha kuwa hadi kufikia sasa ameshatibu wagonjwa wengi walikuwa wakisumbuliwa na magonjwa mbalimbali.

Laizer alisema kuwa dawa hiyo ambayo ameigundua na mpaka kufikia sasa imethibitishwa na wataalamu mbalimbali wa afya pamoja na wakemia mbalimbali wa hapa nchini na hata nje ya nchi.

Aidha amebainisha kuwa mbali na wataalamu hao mbalimbali wa afya kuikubali dawa hiyo pia alishawahi kufanya utafiti wa dawa hiyo kama inafaa katika vituo mbalimbali ikiwemo kituo cha Juhuyu reseache cetre,Bombo reseache ganja fild station,Ubwani reseach ,muhimbili resecher ,Tabora reseach pamoja na centre for enahancemint of effective.

"sasa baada ya kufanya utafiti katika kituo hicho pia nilishawahi kufanya utafiti katika kituo cha utafiti cha serekali ambacho ni kituo cha Ng'ongangare reseacha nao wakanikubali kabisa dawa haina mathara na inafaa"alisema Laizer.

Alibainisha kuwa dawa hiyo ambayo matumizi yake ni siku 30 tu kwa mgonjwa wa ukimwi ndipo hupima na kuonekana kuwa hana maambukizi tena na kwa wagonjwa wasukari hutakiwa kutumia dawa hii kwa siku 14 tu na sukari yao huonekana kuwa sawa pamoja na magonjwa mengine mengi ambayo hupata dozi ya kawaida kuanzia siku tatu hadi saba na mtu hupona moja kwa moja.

Hivyo basi profesa Laizer anasikitishw ana kitendo cha wananchi kuendelea kusumbuliwa na magonjwa sugu wakati yeye anauwezo wa kutibu kwa tiba iliyothibitishwa kisayansi kwa kutumia vipimo vya maabara ambavyo ndivyo vyenye kusema ukweli na kuthibitisha tiba yake anayo itoa hivi sasa katika maeneo ya jengo la makumbusho la Azimio la Arusha.

Kauli hiyo ya mtafiti huyo imekuja baada ya serekali kuwa inatambua kabisa tiba hii kama alivyo eleza katika vyuo hivyo alivyo fanyia utafiti ambapo aliyekuwa naibu waziri wa afya kipindi hicho Muheshimiwa Aisha Kigoda alifika katika kituo cha utafiti cha Ngongongare na kuikubali dawa hiyo na kuhaidi kutengewa bajeti ili isindikwe kitaalamul zaidi kuwanusuru watanzania na nguvu kazi ya taifa katika swala zima la magonjwa hatari likiwemo la ukimwi ambalo limekuwa tishio kwa taifa.

Pamoja na hayo yote mtafiti huyo bado anaiomba serekali iwathamini watafiti wa dawa wa tiba mbadala ambazo zinavirutubisho vingi katika mwili wa binadamu na kuaacha kuthamini dawa zinazotengenezwa viwanda ambazo mara nyingi zimekuwa na kemikali nyingi zinazosabaisha mathara kwa watumiaji .

Akitoa mfano dawa zilizotengenezwa enzi za nyuma kama fansida pamoja nanyingine nyingi ambazo zilikuwa zinatibu malaria lakini watu walipata mathara kutokana na dawa hizo kwani baadhi yao walikuwa wakibabuka ngozi .


Hivyo Mtafiti huyu aliyegundua dawa ya kutibu magonjwa hatari ikiwemo la ukimwi ameishangaa sana na serekali kushindwa kumsaidia kuweza kutoa huduma hiyo kwa uharaka na ukaribu zaidi kwa watu ambao wanasumbuliwa na matatizo mbalimbalil japo kuwa alishawaambia na wanalitambua swala hilo.

Hata ivyo gazeti hili lilibahatika kukutana uso kwa uso na baadhi ya wagonjwa ambao wamepona magonjwa sugu wakiwemo waliopona ugonjwa wa ukimwi ambaye alitumia dozo kwa muda wa siku 30 na kupona kabisa na hivi sasa anafanya kazi zake vizuri baada ya kwenda kwa dakitari katika hospitali ya kibongoto na kupimwa na kukutwa ana maambukizi tena.

Mgonjwa huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Edward Melano(45) ambaye alisema kuwa yeye aligundulika kuwa na maambukizo ya virusi vya ukimwi tangu mwaka 2008 na alianza kutibiwa katika hospitali ya kibongoto kwa muda mrefu akiwa amelazwa lakini mara baada ya kupata dawa ya profesa huyo alipata nguvu na kwenda kupima tena na kugundulika ana maambukizi ya virusi vya ukimwi tena.

Naye mwenyekiti wa kijiji Ng'aritati Abiudi Molel alithibisha kupona kwa mgonjwa huyo na kusema kuwa profesa Laizer amekuwa msaada mkubwa katika kijiji hicho na kwa wagonjwa wa kutoka maeneo mbalimbali ambao wanaenda kupata tiba hiyo kijijini kwake wamekuwa wakimshuhudia kuwa wamepona kabisa na yeye akiwaona kwa macho .

Pia waziri wa wizara ya Afya muheshimiwa Haji Mponda alipokuwa katika mkutano wa watafiti wa tiba mbadala uliofanyika katika jengo la AICC alikubali uwepo wa dawa hiyo baada ya washiriki wa semina hiyo kumuagiza profesa Laizer kuleta dawa hiyo na kuanza kuinywa kwa kutumia vikombe ambavyo vinaujazo wa milimita 300ambayo wanasanyansi walipitisha kutumia hivyo.

Waziri mponda baada yakuona hivyo kwa mujibu wa profesa Laizer alivyoliambia gazeti hili alitoa kauli kuwa atalipeleka serekalini kwani tayari serekali inathamini mchango wa tiba mbadala ambayo imefanywa na chuo cha utafiti cha serekali cha Ngongongare .

Gazeti hili halikuishia hapo liliamua kumtafuata mheshimiwa waziri wa afya Haji Mponda naye alisema kuwa bado hajapata taarifa hizo lakini ataenda ofisini kufuatilia kama kuna taarifa kama hiyo na atatoa maelezo yote pindi afikapo ofisini.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates