BREAKING NEWS

Tuesday, June 21, 2011

WAFANYAKAZI WATAKIWA KUTENGA SIKU YA KUJUMUIKA NA FAMILIA ZAO

WAAJIRI nchini wamekumbushwa kutenga siku maaalum kila mwaka kujumuika na wafanyakazi pamoja na familia zao kupitia michezo Ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji wenye tija katika sehemu mbalimbali za kazi.




Wito huo ulitolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Bia Tanzania TBL na wanafamilia wa TBL wakati wa kuadhimisha siku maalum ya familia kwa watumishi wa kampuni hiyo na familia zao iliyofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ngurdoto iliyopo mkoani Arusha.




Wakizungumza wakati wa maadhimisho ya siku hiyo baadhi ya watumishi na wanafamilia walisema kuwa ufanisi katika sehemu za kazi unaanzia katika ngazi ya familia hivyo ni vyema waajiri nchini wakaelewa umuhimu wa kutenga muda wa kujumuika na wafanyakazi pamoja na familia zao ili kupata fursa ya kukutana pamoja na kubadilishana mawazo kwa njia ya michezo .




Siku hiyo ilipambwa na michezo mbalimbali ikiwemo kukimbiza kuku,kuvuta kamba na kukimbia kwa magunia ilisindikizwa pia na bendi ya mwanamuziki maarufu wa miondoko ya dance nchini Ndanda Kosovo na bendi yake ya maarufu kama "watoto wa tembo".

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates