BREAKING NEWS

Thursday, June 9, 2011

MWENYEKITI AZIRAHI KATIKA KIKOA

KATIKA hali isiyo ya kawaida mwneyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa
CCM(uvccm) wilayani Arumeru mkoani Arusha,Esther Maleko amezirai ghafla na
kuanguka sakafuni na kasha kupoteza fahamu wakati akiwa katika kikao cha kamati
ya utekelezaji cha wilayani humo kilichokuwa kikijadili sakata la vita baina ya
UVCCM na katibu wa CCM mkoa,Mary Chatanda.

Tukio hilo linalohusishwa na imani za kishirikiana na kuzua gumzo mkoani Arusha
lilijitokeza juzi majira ya saa mchana wakati Maleko akishiriki kikao cha
kamati ya utekelezaji wilayani humo kilichofanyika katika ofisi za CCM zilizopo
Sekei wilayani Arumeru.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika zilizolifikia gazeti hili zinadai kwamba mara
baada ya Maleko kupewa nafasi ya kuzungumza ndani ya kikao hicho kuhusiana na
mvutano baina ya Chatanda na UVCCM ghafla alianza kulegea macho na kasha
kudondoka chini sakafuni na kupoteza fahamu hali iliyopelekea kukimbizwa
hospitalini mara moja ili kuchunguzwa afaya yake.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vililiambia gazeti hili ya kuwa Maleko
alinyanyuliwa na kisha kupakiwa haraka ndani ya gari katika zahanati ya Ebel
iliyopo ndani ya kata ya Kaloleni wilayani Arusha.

Mara baada ya mwandishi wa mwandishi huyu alipata taarifa hizo alikimbia mara moja
katika zahanati hiyo kwa lengo la kushuhudia ukweli wa mambo na mara baada ya
kuwasili hospitalini hapo aliwauliza watumishi wa zahanati hiyo na kukiri
kiongozi huyo kufikishwa hapo ambapo walimwelekeza katika chumba alicholazwa.

“Unamuulizia yule dada wa CCM ni kweli yupo hapa wewe nyoosha hapo alafu utakata
kulia kasha nyooka moja kwa moja utamkuta chumbani yuko na ndugu zake huko
uwani”alisema mmojwa wa watumishi wa zahanati hiyo

Mwandishi wa habari mara baada ya kupewa maelezo hayo aliyafuata na kasha
kufika katika chumba alicholazwa na kukuta mlango wa chumba hicho umefungwa huku
sauti za wakina mama wakitoa sala za maombi ikiwa ni pamoja na kukumea mapepo
zikisikika.

Mwandishi wa habari hizi h ilimpasa asubiri nje ya mlango huo ili kujua hatma ya
tukio hilo ambapo sauiti mbalimbali za kukemea mapepo zilisikika zikitamkwa”wewe
pepo shindwa katika jina la Yesu,Bwana Yesu tunaitaka damu ya Yesu Kristo wa
Nazareth ikamsafishe na kukitupa hicho kifaa baharini alichotupiwa”

‘Wewe pepo mbaya mwachie huyu mtoto na familia yake,toka wewe pepo mbaya…toka
pepo ” na sauti nyingine kadha wa kadha


Mara baada ya takribani nusu saa wakinamama wawili walitoka nje ya chumba hicho
na kasha kufuatiwa na wakina mama wengine wawili ambapo mara baada ya baadhi yao
kuhojiwa nje ya zahanati hiyo juu ya sakata hilo walisema kuwa huenda Maleko
alikuwa ametupiwa kitu kibaya wakati akiwa katika harakati za kisiasa bila yeye
kujijua na kupelekea kupoteza fahamu huku wakijigamba ya kuwa hatahivyo tayari
ameshapona

Hatahivyo,mzozo mkubwa ulizuka katika zahanati hiyo mara baada ya ndugu na jamaa
wa karibu na Maleko kubaini ya kuwa kuna baadhi ya waandishi wa habari walifika
hospitalini hapo kujua undani wa tukio hilo ambapo baadhi yao walitishia
kuwapiga na kuwatimua waandishi hao.

Wakati mzozo ukiendelea baina ya ndugu hao na waandishi wa habari Maleko
alionekana akitolewa nje ya zahanati hiyo akiwa ameshikiliwa na ndugu hao huku
akiwa amewekewa bandeji katika mkono wake wa kushoto lakini baadaye taarifa
zilisema kuwa alihamishiwa nyumbani kwa matibabu yake zaidi.

Juhudi za kumpata Maleko ziligonga mwamba kwani simu yake ya mkononi ilikuwa
haipatikani lakini mwenyekiti wa UVCCM mkoani Arusha,James Ole Milya
alithibitisha kiongozi huyo kuanguka wakati akiwa kikaoni huku akisisitiza
kwamba kwa sasa afya yake inaendelea vyema na amesharudishwa nyumbani kwa
matibabu zaidi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates