BREAKING NEWS

Thursday, June 9, 2011

MKUU WA WILAYA KUWA MGENI RASMI KATIKA UZINDUZI WA FILAMU

MKUU wa wilaya Arusha,Raymond Mushi anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa filamu ya Safari ya Yatima (Orphans tour),filamu hiyo imeigizwa na wasanii wa jijini Arusha ikiwa na ujumbe mahususi wa kupiga vita vitendo vya unyanyasaji wanaofanyiwa watoto yatima.



Kwa mujibu wa kiongozi wa kundi la Orphans Tour,Hans Hida alisema kuwa uzinduzi wa filamu hiyo utafanyika kesho( leo) kwenye ukumbi wa Triple A,mjini Arusha,na utahudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali huku wasanii,Nicky wa II, At,Sharomilionea na Bele 9 wanatajaiwa kutumbuiza.



Hata hivyo ,Hida alisema filamu hiyo imetengenezwa kwa kiwango cha mahadhi ya mwafrika na itakuwa ikizungumzia maisha ya watoto yatima ambao wamekuwa wakikusanywa na watu wenyevipato na kisha kujinufaisha kupitia watoto hao.



Alisema maudhuli ya filamu hiyo ni pamoja na kuieleza jamii namna ambavyo athari wanayoipata watoto yatima pale wanapokusanywa kwenye vituo vya kulelea na kujikuta wakitumikishwa bila kupata chochote zaidi ya chakula na mavazi chakavu wanayopatiwa.



Alisema jamii itajionea jinsi watoto yatima wanavyo wanufaisha watu wanaojidai kuwasaidia kumbe wamekuwa wakiwatumikisha ikiwa ni pamoja na kuwauza nje ya nchi kwa lengo na kujipatia malinyingi huku watoto hao wakiteseka kwa kutumikishwa.



Nae msemaji wa kampuni ya Magic Screen Pictures ya jijini dare s salaam iliyotengeneza filamu hiyo,Novatua Lyaruu alisema filamu hiyo imetengenezwa kwa kiwango cha juu cha 3D na inatarajiwa kuanza kuuza mara baada ya uzinguzi huo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates