BREAKING NEWS

Thursday, June 9, 2011

WATAKIWA KUANGALIA UTOAJI WA LESENI ZA UWINDAJI

SERIKALI imeshauriwa kuangalia upya utolewaji wa Leseni za Uwindaji wa wanyama pori nchini kutokana na idadi kubwa ya wanyamapori kuanza kutoweka katika mbuga za hifadhi na kwenye maeneo ya vitalu vya uwindaji ili waweze kuzaliwa tena kwa wingi.



Rai hiyo imetolewa na Luteni msitaafu, Lepirari ole Moreimenti,ambae ni Mratibu wa wafugaji , wahifadhi wa wanyamapori na mazingira ndani na nje ya nchi wa shirika la Hatari Lodge lenye makao yake kijiji cha Momela kinachopokana na hifadhi ya taifa Arusha (Anapa) wilayani Arumeru, kuhusu umuhimu wa kulinda na kuwahifadhi wanyama pori na utunzaji wa mazingira.



Moleimenti,alikuwa kwenye hafla ya kukabidhi zawadi za vinyago vya wanyama mbalimbali wanaopatikana katika hifadhi ya Arusha, kutokana na ubunifu uliofanywa na wanafunzi wa kuchora picha mbalimbali za wanyama wanaopatikana ndani ya hifadhi hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wanafunzi wa shule za awali na msingi katika kulinda wanyama pori na utunzaji wa mazingira.



Watoto hao ambao wanafadhiliwa na mwekezajhi kutoka shirika la Kijerumani la Hatari lodge,lililoko ndani ya hifadhi hiyo ya Anapa, ambapo Moleimenti, amesema kuwa shirika hilo limekuwa msitari wa mbele kuhamasisha na kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira na wanyapori kwa wanafunzi hao.



Moleimenti, amesema kuwa kuna baadhi ya wawindaji wanatumia vibaya Leseni zao kwa kuua wanyama ,majike yenye mimba na madume madogo madogo ambao kisheria hawaruhusiwi kuwindwa, hatua ambayo imesababisha wanyama wengi kutoweka .



Aliwataja baadhi ya wanyama ambao wameanza kutoweka kutokana na uwindaji huo usiozingatia sheria na taratibu kuwa ni pamoja naTandara, Mbuni, pofu, Pongo, Faru, Swala Chorowa Swalatwiga,Duma na Impala.



Ameishauri serikali iwe na Kanda maalumu ya uwindaji ili iweze kumudu kuwafuatilia wawindaji wanaopewa Leseni ili waweze kufahamu aina za wanyama wanaowawinda badala ya kuwaachia wawinde wanavyotaka na matokeo yake baadhi ya wanyama wameanza kutoweka .



Moleiment, ameiomba serikali kuweka Sylabus, ya mafunzo ya uhifadhi wa mazingira na wanyama pori katika mitaala ya elimu ili iweze kufundishwa mashuleni ili kuwalinda wanyama pori hatua ambayo itasaidia wanafunzi hao kuona umuhimu wa kutunza maliasili zilizopo kwa ajili ya vizazi vijavyo.



''Tanzania ni nchi tajiri kutokana na kuwa na maliasili ya wananyamapori na milima ambao hawahitaji viwanda kuwazalishwa kama yalivyo mafuta katika nchi za Uarabuni ambayo iko siku yatakwisha ,lakini wanyama wakilindwa hawatakwisha''alisema .



Nae mkurugenzi wa shirika la Hatari Lodge, Marlies Gabriel , alisema kuwa shirika lake limekuwa likishirikiana na wananchi kuhakikisha wanatunza mazingira na kuwalinda wanyama ndani ya hifadhi hiyo.



Amesema kuwa shirika lake,pamoja na mambo mengine , linajihusisha zaidi na utoaji elimu kwa kizazi kipya cha watoto kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kuwalinda wanyamna pori ambao ni urithi wa kudumu .



Nae mkuu wa hifadhi ya Anapa, Domician Njau, alisema kuwa Anapa, wamejipanga kikamilifu kudhibiti majangili kwa kushirikiana na wanavijiji wanaoizunguka hifadhi hiyo ambayo ipo tangia mwaka 1960 imerkuwa ikikabiliwa na changamoto ya uwindaji haramu hususani Tembo na vifaru tayari wameshatoweka kabisa katika hifadhi hiyo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates