BITEKO AWATAKA MAAFISA UNUNUZI WA UMMA KUFANYA KAZI KWA WELEDI ,UADILIFU NA MAADILI



 Na  Woinde Shizza Arusha


Naibu waziri mkuu Dk Dotto Biteko amewataka maafisa manunuzi na ugavi nchini kufanya kazi zao Kwa uadilifu ,uwajibikaji uwazi na maadili katika utendaji wa kazi na kuepuka vitendo vya rushwa Ili kuonyesha thamani halisi ya matumizi ya fedha za umma


Dk Biteko ameyasema hayo Leo wakati akimuwakilisha Rais Samia Suluhu katika ufunguzi wa Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambapo amesema serikali ya Tanzania imeonesha dhamira yake ya kuimarisha na kuboresha mfumo wa ununuzi wa umma kupitia teknolojia ya kidigitali. 




Aidha alisisitiza umuhimu wa maboresho yaliyofanywa katika sekta ya ununuzi wa umma nchini Tanzania ambapo aliishukuru Wizara ya Fedha pamoja na mamlaka nyingine husika kwa kazi kubwa waliyofanya katika kuboresha usimamizi wa ununuzi wa umma, hasa kwa kuanzisha mfumo mpya wa kielektroniki unaoitwa National e-Procurement System of Tanzania (NeST).


 Alibainisha kuwa Mfumo huu umekuwa msaada mkubwa katika kuongeza uwazi, uwajibikaji, na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma, hasa kwenye miradi ya ununuzi, Katika mfumo wa NeST, taratibu za ununuzi zimeboreshwa na gharama za uendeshaji zimepungua kwa kiasi kikubwa.



Alifafanua kuwa Serikali ya Tanzania imekuwa ikiboresha sheria za ununuzi wa umma kwa lengo la kuongeza thamani ya fedha na kupambana na ubadhirifu wa mali za umma huku alikifafanua kuwa Kwa kupitia maboresho ya sheria ya ununuzi ya mwaka 2023, Serikali imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha kuwa taasisi zote za umma zinatumia mfumo wa kielektroniki wa ununuzi wa umma. 


Kuhusu maendeleo ya ushirikiano wa Afrika Mashariki, aliwataka washiriki wa Jukwaa hili kuhakikisha wanaboresha mifumo yao ya ununuzi wa umma kwa kutumia teknolojia za kisasa ili kuleta tija na ufanisi zaidi huku Akisisitiza kuwa ununuzi endelevu ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kimazingira, hivyo mifumo ya kidigitali inapaswa kuchochea maendeleo haya.




Aidha alitoa wito kwa taasisi zote za umma kuhakikisha zinatumia mfumo wa NeST, huku akisisitiza kwamba taasisi zote zitakazokaidi maagizo haya zitaadhibiwa ,aliwataka washiriki wa jukwaa hili kuhakikisha kuwa wanakuza viwango vya kikanda vya ununuzi endelevu ambavyo vitaimarisha usawa wa kijamii, ukuaji wa uchumi, na uendelevu wa mazingira.


 Kwa upande wake 00 alisema Kongamano la mwaka huu linaongozwa na kauli mbiu isemayo "matumizi ya mifumo ya kidigitali Kwa ununuzi wa umma endelevu"ilikuhakikisha kunakuwa na ufanisi na tija katika manunuzi ya umma serikali ilianza maamuzi ya Kutumia mifumo ya kieletroniki katika ununuzi wa umma nchini kwetu


Alisema mpaka Sasa mifumo miwili imekamilika na mmoja unaendeleaje na inafanya kazi Kwa ufanisi na hadi kufikia  agosti 31 ,2024 jumla ya taasisi nunuzi 1151 ziliweza kuhuisha taarifa zao na kuanza Kutumia mifumo jumla ya taasisi nunuzi 1048 zilitangaza mipango  ya ununuzi ya mwaka.



Kwa upande wake mkurugenzi wa PPRA Denisi Simba alisema kuwa katika jukwaa hilo washiriki watapata fursa ya kubadilishana uzoefu wa namna teknolojia inavyoweza kuleta mabadiliko katika sekta ya ununuzi .



Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post