Ticker

6/recent/ticker-posts

"MAIPAC Yawaongoza Wanawake katika Kuimarisha Uwezo wa Kutetea Haki Zao"

 MAIPAC kuzindua mradi wa kuelimisha ukeketaji kwa watoto wa kike katika jamii ya kifugaji ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa kutetea haki zao.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Shirika la wanahabari la kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) Musa Juma katika ziara iliyofanywa na Asasi za kirai katika wiki ya Asasi hizo iliyofanyika maeneo mbalimbali mkoani Arusha.

"MAIPAC imebaini kuwa watoto wa miaka miwili hukeketwa katika Jamii ya Kimasai hivyo tunampango wa kuzindua mradi wa kuelemisha kuhusu masuala mazima ya ukeketaji na ukatili kwa watoto wa kike , lakini pia kuwajengea Uwezo wa kujiamini wanawake wa kimasai na kuweza kutetea haki zao za msingi hasa katika kukemea Ukatili" amesema.

Katika Ziara iliyofanywa na Asasi za kiraia (CSO) wadau wa asasi hizo wamepata wasaa wakutembelea maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo shughuli za maendeleo zinazofanywa na jamii kwa ujumla huku maeneo yaliyotembelewa na wadau hao ikiwa ni pamoja na Maendeleo ya Jamii Tengeru, Wilaya ya Longido,Kiwanda cha Uzalishaji wa Protini kwa ajili ya Mifugo.

Hata hivyo wiki ya CSO hufanyika mara moja kila mwaka ambapo zaidi ya Wadau 600 wameweza kushiriki na kushirikishana Masuala mbalimbali ya kijamii kwa njia ya midahalo na Majadiliano ya kina yanayolenga Mchango wa ASAS hizo kwa maendeleo ya Taifa.

Post a Comment

0 Comments