Rais Dk Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika kongamano la 16 la wataalam wa maswala ya manunuzi ya umma na ugavi unaotarajia kuanza jumatatu Septemba 9-12 Jijini Arusha.
Kongamano hilo la siku nne linatarajia kufanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mikutano(AICC), na kukutanisha Wataalam wa manunuzi ya umma na ugavi kutoka nchi zote saba za Afrika Mashariki.
Mkutano huo una malengo mbalimbali ikiwemo kujadili fursa za kidigitali katika sekta ya manunuzi ya umma, changamoto na kubadilishana uzoefu lakini pia kupeana mbinu za kukabiliana na changamoto hizo.
Tags
HABARI MATUKIO