Mkutano wa EAPRA Waunganisha Wadau wa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma Afrika Mashariki




 Na Mwandishi wetu , ARUSHA 


Imebainika kuwa taaluma ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma inazidi kupata umuhimu mkubwa katika ulimwengu wa sasa, ambapo uwazi, uaminifu, na mawasiliano yenye manufaa yamekuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. 

Aidha pia   serikali iko mbioni kushirikiana na wadau wa sekta hii kuunda sheria itakayowezesha kuanzishwa kwa Bodi ya Kitaifa ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma  , ambapo itasaidia taaluma hii kupata msukumo wa kisheria na kuwa na mifumo ya usimamizi kama ilivyo kwa taaluma nyingine muhimu kama vile sheria na uhasibu.



Hayo yamebainishwa na naibu waziri wa  habari  mawasiliano Eng.Maryprisca Mahundi wakati akifungua   mkutano  wa jumuiya ya  maofisa mahusiano ya Umma ya AFRIKA Mashariki 
 (EAPRA) uliofanyika leo jijini Arusha, Tanzania, ukikusanya wataalamu na viongozi kutoka sekta ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma.

Alisema kuwa taaluma ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma inazidi kupata umuhimu mkubwa katika ulimwengu wa sasa, ambapo uwazi, uaminifu, na mawasiliano yenye manufaa yamekuwa sehemu muhimu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi. 

Alisema kuwa EAPRA inabaki kuwa kiini muhimu cha kuhakikisha kuwa wataalamu wa mawasiliano wanapata nafasi ya kujenga sauti imara katika vikao vya maamuzi Afrika Mashariki.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa  EAPRA  ambaye pia ni rais wa chama Cha maofisa mahusiano ya Umma Tanzania   Assah Mwambene  alisema kuwa Mkutano huu utafungua njia mpya kwa taaluma hii muhimu kuingizwa kwenye meza za maamuzi na kushiriki katika mchakato wa sera ndani ya ukanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 Alisema kuwa uamuzi wa kuifanya Arusha kuwa makao makuu ya EAPRA, uliofanywa mwaka 2022 katika mkutano uliofanyika Mombasa  na ndio uliweza kufanikisha kuimarisha taaluma hii.

 "Arusha  kama makao makuu ya EAPRA  itasaidia kuinua taaluma ya Mawasiliano na Mahusiano ya Umma kwenye viwango vya juu katika kanda nzima"alibainisha mwambene

kwa upande wa mmoja ya  washiriki ambaye ni mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania (TEF)Deodatus Balile alisema maofisa uhusiano wanakazi kubwa ya kuahakikisha kwamba wanatangaza taasisi zao na sio kubeba mikoba ya mabosi zao.



Aidha aliwataka kutumia nafasi zao kutangaza taasisi zao ili ziendelee kutambulika zaidi  ,nakubainisha kuwa iwapo afisa uhusiano akiwa anaelewa vyema kazi yake nakuifanya vyema  hata bosi wake atamuamini na hatakuwa mkali katika kazi

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post