NCHI YA TÀNZANIA IPO TAYARI KUSHIRIKIANA NA NA NCHI ZINGINE KUIMARISHA MATUMIZI YA MANUNUZI KWA NJIA YA KIDIGITAL:MAJALIWA





Na Woinde Shizza Arusha


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kasimu Majaliwa amesema nchi ya Tanzania iko tayari kushirikiana na nchi nyingine ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuimarisha matumizi ya manunuzi na ugavi kwa njia ya kidigital.


Akifunga Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma Afrika Mashariki lililofanyikabjijini Arusha, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba amesema umuhimu wa sekta ya manunuzi nchini unafanya miradi mbalimbali inatekelezwa.



Aidha Dkt.Nchemba amemuelekeza Katibu Mkuu Hazina kuhakikisha anaratibu na kusimamia sera ya taifa na mkakati wa ununuzi wa umma na ugavi inayofanyika kwenye taasisi za umma zinazingatia misingi ya sera hiyo na mikakati yake ili ianze kutumika mapema.




Mkurugenzi Mkuu wa PPRA Denis Simba amesema kupitia Kauli mbiu katika Jukwaa la 16 la Ununuzi wa Umma katika Nchi za Afrika Mashariki Tanzania imeonyesha mfano wa kuishi kauli mbiu hiyo kwani tayari imeanza kutumia mfumo wa kidigitali na kuanza kuona faida ya matumizi yake katika ununuzi wa umma kupitia mgumo wa Nest.



Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPRA Dkt.Leonada Rafael amesema mada zilizowasilishwa katika mkutano huo zimelenga kuhamasisha matumizi ya Tehama kwenye ununuzi wa umma ili kuweka usawa ,haki, ushindani, uwajibikaji na ufanisi kwenye ununuzi wa umma.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post