OFOO SARO KURUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI MUDA SIO MREFU BAADA YA KUFANYIWA UPASUAJI MKUBWA WA KUSAFISHA TUMBO
arika
na anaweza akaruhusiwa wakati wowote baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa
wa kusafisha tumbo ambao kitaalamu unajulikana kama Toilet Surgery.
Akizungumza
na gazeti hili kwa sharti la kutokutajwa jina, mmoja wa madaktari
katika hospitali hiyo, alisema kwa kawaida upasuaji kama huo ukifanyika
kinachokuwa kinasubiriwa ni mgonjwa kupona vidonda au kupungua kwa
maumivu kabla ya kuruhusiwa.
“Kimsingi
hadi kufanyiwa upasuaji wa namna hiyo ni kuwa ameshatoka katika ile
hali ya hatari na ameshasafishwa na kuondolewa uchafu wote uliokuwepo
ikiwa ni pamoja na kumtibia vidonda vilivyotokana na shambulizi hilo,”
alisema daktari huyo.
Ofisa
Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Eligaeshi alisema Ufoo
anaendelea vizuri na hivi sasa ameanza kula, kufanya mazoezi kidogo na
kujaribu kuzungumza, lakini bado hajaruhusiwa kukutana na watu zaidi ya
ndugu wachache ambao pia wanamwangalia kwa karibu.
Msemaji
wa familia ya Ufoo, Allelio Swai alithibitisha kutengemaa kwa hali ya
mwandishi huyo.Swai alisema Ufoo hivi sasa anaendelea vizuri na
madaktari wamewaeleza kuwa wakati wowote anaweza akaruhusiwa
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia