HALMASHAURI YA MERU YAWEKA BIKONI KATIKA MIPAKA YOTE ILIYOPO KATIKA VYANZO VYOTE VYA MAJI PAMOJA NA KUOTESHA MITI 7000

Afisa mifugo ya meru Dr. Amani Sanga akizungumza katika  kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani na wananchi wa  kijiji cha Ngyani kilichopo katika kata ya Nkwaranga ndani ya  halmashauri ya meru   niaba ya mgeni ramsi ambaye mkuu wa wilaya ya meru
Afisa Maendeleo ya Jamii wa  bonde la pangani Abraham Yesaya akiwa anaelezea shughuli ambazo wanazifanya wao kama bonge la pangani

Woinde Shizza, Arusha


WAKATI Mataifa mbalimbali yanaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani iliofikia kilele chake hapo Jana Juni 5, 2018, halmashauri ya wilaya ya Meru imeathimisha kwa kupanda miti 7000 huku miti 500ikiwaimepandwa katika siku ya kilele chamaathimisho haya Pamoja na kuweka bikoni katika mipaka inayozunguka vyanzo vya maji vilivyopo ndani ya halmashauri hiyo. 


Kwa miaka mingi siku ya Mazingira duniani imekuwa ikiadhimishwa kwa Wadau katika nchi mbalimbali kuchukua hatua chanya zinazohusu mazingira. Siku hii pia imekuwa ni sehemu ya kampeni ya utoaji elimu juu ya maswala yanayojitokeza kuhusiana na mazingira.


Kauli mbiu katika maadhimisho ya mwaka huu inasema “MKAA NI GARAMA TUMIA NISHATI MBADALA” ikihamasisha jamii kuwa na urafiki endelevu na mazingira asilia ambapo kila mtu anapaswa kutambua, kufurahi, kujivunia na kulinda uzuri wa mazingira asilia na kuhamasishana ili kuyatunza na kuyahifadhi.


Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira duniani Afisa mifugo ya meru Dr. Amani Sanga Kwanza niaba ya mgeni ramsi ambaye mkuu wa wilaya ya meru alisema Kuwa Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingi Barani Afrika na duniani kwa ujumla imeendelea kuathirika kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa mazingira unaotokana na shughuli mbalimbali zikiwemo za kilimo, ufugaji, ujenzi n.k


Uharibifu huu wa misitu hutokana na shughuli za kilimo na ufugaji kwa njia zisizo endelevu. Uharibifu huu wa misitu unachangia pia kukosekana kwa mvua, kukauka kwa mito, mabwawa na uoto wa asili.


 Aisha alibainisha kuwa kazi ya kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira inahitaji ushirikiano wa Wadau katika ngazi zote.


Alisema halmashauri ya Meru katika kuazimisha siku hii imepata ushirikiano kutoka Kwa wadau mbalimbali wakiwemo bonde la pangani, mali hai klabu,kili flora, mamlaka ya making  mjimdogo wa usa river Pamoja na SUAMA. 


  Taasisi na Asasi za Kiraia zikishirikiana  katika kutekeleza kikamilifu Sheria na Kanuni za uhifadhi wa mazingira nchini ili  in a inasaidia kupunguza kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.


Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii wa  bonde la pangani Abraham Yesaya alisema Kuwa Katika kilele cha maadhimisho haya Wametoa jumla ya miti 7000 ambayo imepandwa katika Kata 12 na kutoa elimu ya misitu katika shule zaidi ya 20.
Alisema ni wajibu wa mamlaka katika ngazi mbalimbali ziwe na Mipango bora ya ardhi, mikakati ya uhifadhi wa vyanzo vya maji, pamoja na udhibiti wa uvunaji holela wa misitu na ufugaji usio endelevu Pamoja na kutoa elimu juu umuhimu wa kutunza mazingira na faida zinazopatikana ili Wananchi waunge mkono jitihada zinazofanywa katika kulinda na kuhifandhi mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.


 “Usafi wa mazingira uhusishe kila mtu kuhakikisha taka haswa Za plastiki zinakusanywa na zinatupwa katika maeneo yaliyotengwa na tupande miti mingi wakati wa msimu wa mvua ili tujihami na kuenea kwa hali ya jangwa na mabadiliko ya tabianchi” alisema Yesaya
Alisema, maliasili zilizopo  zinahitajika kwa matumizi ya vizazi vilivyopo na vijavyo, hivyo uwepo wake hutegemea zaidi uhifadhi wa rasilimali hizo na  matumizi katika jamii iliopo na ijayo.


kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji cha Ngyani kilichopo katika kata ya Nkwaranga katika halmashauri ya meru Elishilia Mathayo alisema anashukuru sana halmashauri ya meru kwakuwaekia mipaka na bikoni katika kwenye maeneo ya vyanzo vya maji kwani hii itasaidia kuonyesha wananchi wanaofanya shughuli  za kibinadamu Kujua mipaka yao ya kufanya shughuli hizo na hii itasaidia  kuendelea kutunza vyanzo vyetu vya maji 


 Alisema Kama ilivyo Madhumuni ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ni kuhamasisha jamii kuelewa masuala yahusuyo mazingira na kuchukua hatua za kuhifadhi na kulinda mazingira na kama Kauli Mbiu iliyoongoza maadhimisho haya kimataifa ni “tokomeza uchafuzi wa plasicki”,  huku kitaifa Kauli mbiu ikiwa inasema "mkaa gharama tumia nishati mbadala."

lengo likiwa ni kuhamasisha utunzaji wa mazingira hivyo niwajibu wa kila mtu kutunza mazingira na mazingira yamtunze.

 mgeni rasmi akipanda moja ya miti
 baadhi ya wadau wa SUAMA wakisikiliza hutuba ya mgeni rasmi mara baada ya kufanya zoezi la uhoteshaji miti
 mwenyekiti wa kijiji cha Ngyani kilichopo katika kata ya Nkwaranga katika halmashauri ya meru Elishilia Mathayo akizungumza katika maadhimisho hayo
 mmoja wa wananchi ambaye jina lake halikufahamika akitoa dukuduku lake mbele  ya mgeni rasmi ambapo aliomba zoezi hili la upandaji miti liwe endelevu
 mbali na upandaji miti pamoja na uelimishaji juu ya utunzaji wa mazingira pia halmashauri ya meru kwa kushirikiana na bonde la pangani waliandaa maonyesho ya majiko mbalimbali ambayo yanatunza mazingira kama kauli mbiu inavyosema mkaa ni gharama tumia nishati mbadala

About woinde

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia