
Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege
ameridhishwa na matumizi ya fedha kwenye ujenzi na uboreshaji wa Kituo
cha Afya Usa- River na kueleza kuwa thamani ya fedha imeonekana pia
ametoa wito kwa Halmashauri nyingine kuiga mfano.
Mhe.Naibu Waziri Kandege amesema hayo alipokagua ujenzi na ukarabati
wa kituo cha Afya Usa- River wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa vituo
vya Afya vilivyopewa fedha na Serikali kwenye Mkoa wa Arusha kwaajili ya
ujenzi wa majengo mapya na kukarabati yaliyopo kwa lengo la kutoa
huduma bora za Afya, pia Mhe.Naibu Waziri Kandege amemwagiza Mganga
Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt. Cosmas Kilasara kutoa elimu
ya kina kwa wananchi ili waweze kujiunga na mfuko wa Afya ya jamii CHF.
Aidha ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwenye kituo hicho cha Afya
Usa -River ni baada ya Serikali kutoa fedha kiasi cha Sh. milioni 500
kwa ajili ya kuboresha kituo hicho kwa kujenga majengo mapya ambayo ni
jengo la maabara,nyumba ya mtumishi, jengo la upasuaji, wodi ya mama na
mtoto, chumba cha kuifadhia maiti, kichomea taka pamoja na kufanya
ukarabati wa majengo yaliyokuwepo kwa lengo la kuwapa wananchi huduma
bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege(wakwanza
kulia) akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Wilaya ya
Arumeru, Ndg.Timotheo Mzava,Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya
ya Meru Ndg.Christopher Kazeri,Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt.
Timoth Wonanji ,Mganga mkuu wa Halmashauri ya Meru Dkt. Cosmas Kilasara
pamoja na wataalamu wenginewakitembelea na kukagua ujenzi kwenye kituo
cha Afya Usa-River.

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la Upasuaji kwenye kituo cha Afya Usa-River.

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la Upasuaji kwenye kituo cha Afya Usa-River.

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la kuwahudumia wagonjwa wa wa nje (OPD)

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea jengo la kuwahudumia wagonjwa wa wa nje (OPD)

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege
alipotembelea jengo la wodi ya mama na mtoto kwenye kituo cha Afya
Usa-River.

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege
alipotembelea sehemu ya kufulia iliyopo kwenye wodi ya mama na mtoto
kwenye kituo cha Afya Usa-River.

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege alipotembelea kichomea taka katika Kituo cha Afya Usa-River.

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege akikagua upauzi wa njia ya kuptia wagonjwa .

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege akitoa mrejesho wa ukaguzi wa kituo cha Afya Usa-River.

Naibu waziri Ofisi ya Raisi TAMISEM mhe. Josephat Kandege
akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru
Christopher Kazeri .