
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto
Mhe.Dkt. Faustine Ndugulile amepongeza Halmashauri ya Wilaya ya Meru kwa
kusimamia vyema ujenzi na uboreshaji wa Kituo cha Afya Usa- River
uliolenga kuboresha upatikanaji wa huduma za afya katika umbali mdogo
na kupunguza msongamano kwenye Hospitali ya Wilaya Meru iliyopo Tengeru
na Hospitali ya Rufaa Mount Meru.
Mhe.Naibu waziri Ndugulile amesema hayo alipokuwa kwenye ufuatiliaji
wa utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa wakati alipo fanya ziara kwenye
Halmashauri ya Wilaya ya Meru ya hali upatikanaji wa dawa kwenye vituo
vya Afya na zahanati na kufurahishwa na utekelezaji uliofanyika .
Aidha Mhe.Ndugulile amesema Serikali ya awamu ya tano imeipa
kipaumbele Afya ya mwananchi kwa kuhakikisha anapata huduma bora za afya
kwenye umbali unaofikika hivyo baada ya ujenzi na uboreshaji wa vituo
vya Nchini Serikali inatatua changamoto ya uhaba wa watumishi wa Afya
kwani mpaka sasa imetoa kibali cha kuajiri watumishi wa afya wapatao
8000 kati yao 6,200 wataajiriwa kwenye mamlaka za Serikali za mitaa.
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher Kazeri
ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha milioni 500 iliyotumika kuboresha
kituo hicho cha Afya Usa - River kwa kufanyika ujenzi wa majengo mapya
ambayo ni jengo la maabara,nyumba ya mtumishi, jengo la upasuaji, wodi
ya mama na mtoto, chumba cha kuifadhia maiti, kichomea taka pamoja na
kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo ambayo ni Jengo la kuwahudumia
wagonjwa wa wa nje (OPD), jengo la duka ambalo awali lilitumika kama
kama jengo Maabara,Jengo lenye pande mbili likitumika kama wodi ya
wanawake na wanaume .

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe
Dkt. Faustine Ndugulile pamoja na viongozi wengine akikagua ujenzi na
uboreshaji wa kituo cha Afya Usa- River.

Mganga mkuu wa Mkoa wa Arusha Dkt. Timoth Wonanjina Mganga Mkuu wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Dkt.Cosmas Kilasara wakitoa ufafanuzi kwa
Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt.
Faustine Ndugulile

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Dkt. Faustine Ndugulile

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe
Dkt. Faustine Ndugulile akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa kwenye
Kituo cha Afya Usa - River.

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe
Dkt. Faustine Ndugulile akimuhoji mama mgonjwa juu ya huduma ya dawa
kwenye kituo cha Afya Usa- River.

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe
Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na Katibu Tawala kwenye Wilaya ya
Arumeru Timotheo Mzava juu ya utekelezaji wa maagizo ya ziara yake ya
awali.

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe
Dkt. Faustine Ndugulile akipongeza namna ujenzi na uboreshaji wa Kituo
cha Afya Usa- River ulivyosimamiwa vyema .

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe
Dkt. Faustine Ndugulile akimuhakikishia Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Meru imetekeleza Ujenzi huo na ukarabati wa Kituo cha Afya
Usa- Rive kama Serikali ilivyokusudia.

Naibu waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe
Dkt. Faustine Ndugulile akimpa mkono wa pongezi Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Meru Christopher Kazeri usimamizi mzuri Ujenzi
huo na ukarabati wa Kituo cha Afya Usa- Rive kama Serikali
ilivyokusudia.