Ticker

6/recent/ticker-posts

MFUMO MPYA KUTUMIKA KUPANGA VITUO VYA KAZI KWA WATUMISHI




Katibu tawala msaidizi Mkoa wa Mbeya anayesimamia Utawala na Rasilimali watu, Marco Masaya akifungua mafunzo ya mfumo mpya wa kuwapangia vituo vya kazi watumishi wa idara ya afya yaliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Usungilo.

Mkuu wa timu ya Mifumo ya Rasilimali Watu kutoka PS3, Dk. Josephine Kimaro (kushoto) akiendelea na majukumu yake katika ukumbi wa Usungilo wakati wa mafunzo kwa wakuu wa Idara za Afya wa Halmashauri za Mkoa wa Mbeya.Washiriki wa Mafunzo wakiwa kwenye majadilianoWashiriki wa mafunzo wakifanya kazi kwa vitendo kuhusiana na mfumo mpyaWaganga wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mbeya wakifuatilia kwa makini mafunzo juu ya namna ya kupanga vituo vya kazi kwa watumishi wa Idara ya afyaWatumishi wa Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Mbeya wakifuatilia mafunzo ya namna ya kupanga vituo vya kazi kwa watumishi.

SERIKALI imeanzisha mfumo mpya wa kuwapangia vituo vya kazi watumishi wapya wenye lengo la kuangalia mahitaji pamoja na utendaji kazi wao.

 

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa timu ya Mifumo ya Rasilimali Watu kutoka Mradi wa uimarishaji wa mifumo ya sekta za umma (PS3), Dk. Josephine Kimaro wakati wa mafunzo kwa Waganga wakuu wa Wilaya, Maafisa Utumishi, Makatibu wa afya na watunza taarifa za afya wa ngazi za Halmashauri na Mkoa wa Mbeya yanayofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Usungilo jijini Mbeya.

 

Josephine alisema mfumo huo unaojulikana kwa jina la WISN (Workload Indicator of Staffing Needs) na POA (Prioritization Optimisation Analysis) utasaidia kubaini utendaji kazi wa watumishi baada ya kupangiwa kwenye kituo cha kazi.

 

Aliongeza kuwa mfumo huo pia husaidia kubaini mahitaji ya watumishi katika Zahanati na Kituo cha Afya kulingana na uzito wa kazi zinazohitajika hivyo kumsaidia msimamizi wa kituo kuomba watumishi kwenye mahitaji zaidi.

 

Awali akifungua mafunzo hayo, Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Mbeya anayeshughulikia Utawala na Rasilimali watu, Marco Masaya alitoa wito kwa Makatibu wa Afya kuzingatia matumizi ya mfumo huo baada ya mafunzo.

 

Alisema Serikali inatarajia kuanza kutoa watumishi wa idara ya afya kupitia mfumo huo mpya Juni 1 hadi 7 mwaka huu hivyo  wahusika wajiandae kuwapokea kulingana na utaratibu.

 

“Kuanzia tarehe moja hadi tarehe saba tutaanza kupokea watumishi wapya kupitia mfumo huu hivyo kama kuna aliyedanganya bora ajirekebishe mapema ili kuepuka usumbufu kwa mtumishi huyo” alisema Masaya.

 

Aliongeza kuwa pia Wakuu wa Idara wanatakiwa kufuata muongozo unaoelekeza namna ya kumpokea mtumishi mpya kabla ya kumpeleka katika kituo cha kazi.

 

“Hivi sasa kuna muongozo umetolewa na serikali wa namna ya kuwapokea watumishi wapya hatua za kufuata kabla ya kumpeleka katika kituo cha kazi hivyo tufuate utaratibu huo” alisisitiza Masaya.

 

Alisema kulingana na muongozo huo, Mtumishi mpya anapaswa kuelekezwa hali halisi ya kituo chake cha kazi ikiwemo hali ya hewa watakaompokea na atakaofanya nao kazi jambo linaloweza kumsaidia kujiandaa kisaikolojia

Post a Comment

0 Comments