Warembo wanaoshiriki mashindano ya kumsaka mlimbwende Miss Arusha mwaka 2018 wametakiwa kuweka mbele Taswira ya taifa na kutafsiri kuwa mashindano hayo ni sawa na kazi zingine
Akizungumza Mapema leo Juni 5,katika uzinduzi wa mashindano hayo Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqaro aliwataka washiriki katika mashindano hayo kuonyesha jamii kuwa ulimbwende sio.uhuni Bali kazi inayoweza kulitangaza taifa kupitia vivutio vyake
"Tunatamani kuona vijana wakijikita katika fursa kama hizi badala ya kukaa vijiweni na katika makundi yasiyofaa,lakini kupitia kazi hii mnaweza kuionyesha jamii kuwa hii nayo ni miongoni mwa kazi"alisema Daqaro.
Mkurugenzi wa mashindano hayo, Tilly Chizenga alisema walipotangaza kuwepo kwa mashindano hayo walijitokeza warembo 70 kushiriki ambapo waliwekwa katika makundi na baada ya mchujo walipatikana 20 wanaotarajia kuanza kambi julai 6 mwaka huu.
Katika Kambi hii watakuja na kurudi majumbani hawatalala lakini pia tumeandaa wataalamu mbalimbali kuwapatia Mafunzo wakiwemo wataalamu wa afya,watapata elimu ya kisaikolojia pamoja na kufundishwa mambo ya kiroho"Alisema Chizenga.
Alisema washindi watatu wataibuka na zawadi mbalimbali ambapo mshindi wa kwanza atapatiwa sh,1 milioni, mshindi wa pili atanjinyakulia sh,700,000 na mshindi wa tatu atakabidhiwa sh,500,000.