Askofu MKUU wa Kanisa Katoliki jimbo kuu LA Arusha,Isaac Amani amepiga Marufuku Kwa maharusi wa kike mwenye ujauzito kuvaa Shela wakati wa kufunga ndoa kanisani
Aidha Askofu huyo pia amezuia kufanyika kwa sherehe za ubarikio ,ubatizo na komunio kwenye kumbi za starehe.
Askofu Amani ametoa utaratibu huo mpya mapema leo, jumapili April 29, wakati wa misa takatifu ya shukrani aliyoitoa kwa waumini wa kanisa hilo iliyofanyika katika kanisa katoliki LA mt,Thereza jijjni Arusha.
Jambo hilo limepokelewa Kwa mtazamo tofauti na waumini hao huku wengi wao wakishangilia na baadhi yao wakiduwaa.