Taasisi ya habari kusini mwa Afrika tawi la Tanzania(MISA-TAN),imeiomba serikali kupunguza viwango vya ada ya kuendesha mitandao ya kijamii(Blogs,Online Tv na You Tube ili kuvutia vijana wengi kumiliki.mitandao kisheria.
MISA pia imeomba serikali kuharakisha kuunda baraza huru la habari na mfuko wa
kusaidia wanahabari nchini kujiendeleza kielimu.
Mjumbe wa bodi ya MISA-Tan,Mussa Juma ametoa wito huo leo June 26, wakati akifunga Warsha ya waandishi wa habari na wadau wa habari kujadili kanuni za maudhui ya mtandaoni za mwaka 1998 na maboresho yake katika hotel ya Silver sand kunduchi jijini Dar es salaam.
Warsha hiyo iliandaliwa na MISA-Tan kwa ushirikiano na Shirika la Protection international Afrika na kudhamiwa na serikali ya Finland.
Juma alisema, gharama.ya sh 500,000 ya lesseni ua kumiliki blogs na millioni mona kumiliki luninga za mtandaoni ni kubwa kwa vijana na watu wenye ulemavu.
"Kama ada ya lesseni ikiwa ndogo vijana wengi wenye taaluma ya habari na TEHAMA watamiliki mitandao ya kijamii kisheria na kutoa habari"amesema
Amesema kwa sasa kutokana gharama kubwa za leseni karibu tobo tatu ya mitandao inaendeshwa bila lesseni .
Alisema muhimu serikali kupitia TCRA kugawa mitandao ya jamii ambayo inamilikiwa kibiashara na ambayo inafanya kazi ya kutoa elimu na kupashana.habari pekee.
Juma ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari(JOWUTA) na mkurugenzi wa taasisi ya wanahabari ya MAIPAC, pia aliomba serikali kuharakisha kuudwa baraza huru la habari,bodi ya ithibati na mfuko wa kusaidia wanahabari.
Akizungumza kwa niaba ya Msemaji mkuu wa serikali,Mkurugenzi msaidizi wa Maelezo,Patrick Kipangula alisema serikali kupitia TCRA bado inaendelea na utafiti juu ya masuala ya lesseni na ada mbalimbali.
Kipangula hata hivyo aliwataka wanahabari ma wadau wa habari kuheshimu sheria na kanuni za masuala ya habari .
Awali wakitoa mada katika warsha ,Mawakili Gedion Mandes , Afisa programu wa LHRC Raymond Kanegene na Deus Kibamba walitaka wanahabari na kusoma kanuni za maudhui ya mitandaoni ili kutovunja sheria.
Wakili Mandes pia licha ya kushauri kupunguzwa ada za leseni alitaka elimu zaidi kutolewa juu ya kanuni hizo na kuzingatia haki za makundi ya walemavu.
Wakili Kanegene akichambua kanuni hizo alisema zinamapungufu lakini lazima zifuatwe.
Alibainisha mapungufu ikiwepo kukataza kuandika habari za kuchochea biashara ya kamari mitandaoni wakati serikali ikipokea kodi.
Kwa upande wake Kibamba alisema.lengo la kanuni za maudhui mtandaoni ni kudhibiti usambazaji holela wa habari na taarifa.
Katika kanuni hii kuna mambo mazuri na mabaya hivyo ni muhimu kuzijua kanuni.
Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi wa MISA TAN Elizabeth Riziki alisema MISA itatumia njia ya majadiliano ma serikali na wadau katika kudai kanuni nzuri za maudhui ya mitandaoni lakini pia sheria bora.
Alisema anaishukuru serikali ya awamu ya sita walau imeboresha baadhi ya sheria na kanuni na imefungua milango ya majadiliano zaidi ili kuboresha uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.
Zaidi 33 kutoka Tanzania bara na visiwani walishiriki warsha hiyo.