WANAWAKE GOMBEENI SERIKALI ZA MITAA - REGINA NDEGE

 


Na Mwandishi wetu, Kiteto

WANAWAKE Mkoani Manyara wametakiwa kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi ujao wa serikali za mitaa.


Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara, (CCM) Regina Ndege ametoa wito huo kata ya Kibaya wilayani Kiteto, wakati akizungumza kwenye kikao cha baraza la umoja wa wanawake (UWT) wa wilaya hiyo.




Ndege amesema wanawake wasibaki nyuma kwenye kushiriki uchaguzi ujao wa serikali za mitaa hivyo wajitokeze katika kugombea kwani wana uwezo mkubwa.



"Wanawake tunapaswa kuaminiana, kujuliandaa na kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuomba nafasi mbalimbali za uongozi," amesema Ndege.



Amesema wanawake wasijihisi wanyonge kwani wanapaswa kufuata nyayo za Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika uongozi.



"Tusihofie chochote wanawake tuna uwezo mkubwa wa uongozi kwani hata nchi ipo mikopo salama ya Rais Samia na hapa Manyara tuna mwana mama mahiri mkuu wetu wa mkoa Queen Sendiga," amesema Ndege.



Amesema anatarajia kwenye mkoa huo watajitokeza wanawake wengi katika kugombea nafasi za uongozi kuanzia ngazi ya vijiji, vitongoji na mitaa.



"Naomba wanawake wenzangu tujenge Imani ya kuaminiana na tuungane mkono tuache tabia ya kutoaminiana," amesema Ndege.



Mmoja kati ya wajumbe wa kikao hicho, Ngaisi Mollel amesema ujumbe huo ni mzuri kwa wanawake ili nao waweze kuchukua nafasi za uongozi.



Mollel amesema watafikisha ujumbe huo hadi kwenye ngazi ya vitongoji ili wanawake wengi zaidi wahamasike kugombea nafasi hizo.



"Tunatarajia wanawake wengi zaidi kujitokeza kugombea nafasi za kugombea uongozi wa serikali za mitaa pindi muda wa

 uchaguzi utakapofika," amesema.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post