Wananchi wanashauriwa kutumia OONI kwa sababu ni zana ya bure inayowezesha watumiaji kupima upatikanaji wa mtandao na huduma za mtandaoni, ikitoa taarifa muhimu kuhusu hali ya uhuru wa mtandao katika maeneo mbalimbali.
Hayo yameelezwa katika warsha ya siku mbili ya wanawake kutoka asasi za kiraia pamoja na waandishi wa habari ilioandaliwa na taasisi ya Zaina foundation ambapo alibainika kuwa OONI (Open Observatory of Network Interference) ni mradi wa kimataifa unaolenga kufuatilia, kugundua, na kuripoti udhibiti wa mtandao na vizuizi vya tovuti.
kazi ya Kwanza ya OONI inasaidia kuelewa hali halisi ya upatikanaji wa mtandao nchini ambapo alisema Kupitia vipimo vya OONI, watumiaji wanaweza kugundua kama tovuti au huduma fulani zinadhibitiwa au kuzuiwa na mamlaka na hii inasaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji wa serikali na watoa huduma za mtandao.
Pia OONI inachangia katika juhudi za kimataifa za kulinda uhuru wa mtandao, Data zinazokusanywa kupitia OONI zinatumika katika tafiti na ripoti za kimataifa kuhusu hali ya upatikanaji wa mtandao ambapo inasaidia mashirika na watetezi wa haki za dijitali kuboresha sera na mikakati ya kulinda uhuru wa habari na habari mtandaoni.
kwa kutumia OONI, wananchi wanapata uelewa zaidi kuhusu haki zao za kidijitali na umuhimu wa uhuru wa mtandao na inachochea uelewa na ushiriki wa wananchi katika masuala ya kidijitali, na hivyo kusaidia kujenga jamii yenye uelewa na inayotetea haki za mtandaoni.
Alibainika kuwa , ni muhimu kwa wananchi kutumia OONI ili kufuatilia, kuripoti, na kulinda uhuru wa mtandao, na hivyo kuchangia katika kujenga mtandao huru na salama kwa wote.