Hesabu Tanzania (NBAA) imewahimiza vijana wa kitanzania nchini kuchangamkia fursa za Uhasibu na Ukaguzi kutokana na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo endelevu ya Taasisi, makampuni ili kuleta tija kwenye ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Taifa.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu Jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.
"Tunasimamia vigezo vya uandaji wa hesabu za kimataifa na kuhakikisha wanachama wetu wanazingatia maadili na vile vigezo ambavyo vinafanya tasnia ya uhasibu iwe na heshima na mchango unaotarajiwa na wananchi" amesema CPA Prof. Sylvia Temu
Prof. Sylvia Temu ameongezea kuwa ushiriki wa NBAA katika maonyesho haya umesaidia kutoa elimu na kusikiliza sana wadau ili kupata maoni mbalimbali na kutoa mrejesho juu ya kazi zinazofanywa na NBAA ili kuboresha zaidi kazi zetu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya alipotembelea banda la Bodi hiyo lililopo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayofanyika katika viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, Temeke, jijini Dar es Salaam. Wa Kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Shirika kutoka NBAA CPA Kulwa Malendeja.
Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Bodi hiyo.
Tags
HABARI MATUKIO