Wafanyabiashara wa barabara wapewe wiki kuondoka na Mkuu wa Wilaya Arusha
Na Woinde Shizza,Arusha
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Joseph Mkude, amewaambia wafanyabiashara wakubwa na wadogo (machinga) waliovamia barabara kufanyia biashara, kwamba waondoke ndani ya wiki moja.
Amesema hayo leo wakati akitembelea soko la Kariakoo kuangalia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara, Ziara hiyo ililenga kuona kilichosababisha wafanyabiashara kutumia barabara kama sehemu ya biashara.
Mkude amesisitiza kwamba biashara ifanyike tu katika maeneo yaliyoidhinishwa na kwamba wafanyabiashara wafuate sheria na taratibu zilizowekwa.
Aidha, aliwataka wafanyabiashara wadogo wapya ambao hawana sehemu rasmi za biashara kuwasiliana na ofisi za halmashauri ili wapangiwe maeneo rasmi ya kufanya biashara

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia