RC MAKALLA AKUTANA NA WAMILIKI WA MABASI UTATUZI WA FOLENI ARUSHA
_Wakubaliana kupunguza Foleni na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi_
_Wamiliki wa mabasi wamshukuru Rais Samia kwa ujenzi wa Stendi kubwa na ya kisasa Bondeni City_
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla leo Jumanne Januari 27, 2025 amekutana na Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) na mamlaka za serikali zenye kusimamia miundombinu, usalama na Mipango Miji Jijini Arusha, wakikubaliana kwa pamoja kuchukua hatua za kuondoa foleni Jijini Arusha ili kutoathiri shughuli za utalii, kiuchumi na kijamii.
Kulingana na Mhe Makalla, Wajumbe wa Kikao hicho pia wamekubaliana kuboresha huduma za usafirishaji kwa wananchi wa Mkoa wa Arusha, pamoja na maandalizi ya kuhamia kwenye Kituo kipya cha mabasi cha Bondeni City pale kitakapokamilika, akitoa wito kwa Uongozi wa Jiji kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na usalama kwenye Kituo cha Mabasi cha sasa.
Kwa upande wao Wamiliki wa Mabasi wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa Kituo kipya cha mabasi, wakiahidi pia kushirikiana katika kutekeleza kikamilifu mikakati waliyojiwekea ya kupunguza foleni na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi, wakihimiza zaidi matumizi ya tiketi mtandao kwa wananchi ili kuepusha usumbufu na foleni katikati ya Jiji la Arusha.




0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia