UONGOZI wa kampuni ya Utalii ya Tanganyika Film tawi la Ndarakwai Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro umesema kuwa umekusudia kuimarisha sekta ya michezo kwa lengo la kuwawezesha vijana katika wilaya hiyo katika harakati za kuimarisha michezo.
Meneja wa Kampuni hiyo tawi la Ndarakwai, Thomas Olekuya alisema hayo wakati akizungumza na wachezaji wa timu ya Roseline FC na kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya michezo kwa la kuimarisha michezo katika kata ya Ndumeti wilayani hapo kwenye kikao kilichofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Roseline.
Alisema, kampuni yake imeamua kuimarisha timu moja ya ndani ya kata hiyo jambo ambalo litarahisisha hata upatikanaji wa vifaa na misaada kwa wepesi zaidi kuondoa tatizo sugu la upatikaji wa vifaa vya michezo
.
"Ndugu wachezaji wa timu hii ya Roseline nawaahidi kuwa
nitahakikisha kwamba Sekta ya Michezo inapata nguvu zaidi kutokana na umuhimu wake uliojichomoza hivi karibuni wa kutoa ajira endapo Vijana hao watajituma vilivyo."alisema Olekuya
Alisema suala la kuimarisha michezo litakwenda sambamba na
upatikanaji wa vifaa vya michezo ikiwemo Mipira, Nyavu Magoli na Jezi ambapo alisema zimo ndani ya uwezo kampuni kulingana na utaratibu aliouweka wa kusaidia vijana kupitia michezo
Akipokea vifaa hivyo vya michezo kwa niaba ya wachezaji wa timu hiyo diwani wa kata ya Ndument , Charles Mwaijage aliishukuru kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kutatua changamoto zinazowakabili katika sekta ya michezo ikiwa ni pamoja na uhaba wa vifaa vya michezo ya aina mbalimbali
Diwani huyo alisema kutatuliwa kwa changamoto hizo kutawawezesha Vijana walio wengi wa jimbo hilo kuepuka kusambaratika pamoja na vishawishi vinavyoweza kuwapelekea kujiingiza katika matendo maovu.
Hata hivyo Meneja huyo alikabidhi seti ya Jezi, mpira,vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja kwa timu hiyo pamojana kuwaahidi kuwapatia viatu kwa ajili ya kujiandaa na mashindano mbalimbali yatakayoanza wilayani hapo