tuserebuke kwa ushindi jamani chezea mailstone park wewe
wafanyakazi wa mailstone wakisherekea pamoja na meneja wao alievaa nguo nyeusi mara baada ya kupokea kikombe
Mchoma nyama maarufu akiwa amebibwa na wafanyakazi wenzake wa bar ya milestone park mara baada ya kutangazwa washindi
Milestone Park wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Safari Lager Nyama Choma 2014 yaliyofanyiaka mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa General Tyre jijini Arusha na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja(1,000 000/=) na Kikombe.
Mshindi wa pili katika fainali hizo ni QX Pub ambao walizawadiwa fedha taslimu shilingi laki nane (800,000/=), mshindi wa tatu ni Royal Stop Over Bar ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki sita (600,000/=), mshindi wa nne ni New City Garden ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki nne (400,000/=) na nafasi ya tano ilichukuliwa na Arusha Raha Bara ambao walizawadiwa fedha taslimu Shilingi laki mbili (200,000/=)Akizungumza na wakazi jiji la Arusha waliohudhuria fainalihizo, Mkuu wa Opaeshen wa jiji la hilo, ASP.Edward Balele aliwashukuru kampuni ya bia Tanzania(TBL) kwa kuanzisha mashindano hayo yenye mvuto wa pekee na yenye kutoa ajira na kukuza kipato kwa wachoma nyama,lakinipia alizipongeza bar tano zilizochaguliwa kwakura za wateja wao kuwa ni bora na kufanikiwa kushiriki fainali hizo.Alisema Balele katunzeni na kulinda hadhi hii na kidogo mtakachopewa na Safari Lageer kama zawadi mkakitumie vyema kuboresha majiko yenu