Chama cha upinzani MSD chake Alexis Sinduhije kimezuiwa kuendelea na shughuli zake kwa miezi minne
Umoja wa mataifa na Muungano wa Ulaya zimeelezea
wasiwasi kuhusu mvutano wa kisiasa unaozidi kutokota kati ya serikali na
vyama vya upinzani nchini Burundi.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon,
amelaani hali ya kisiasa nchini humo,akisema kuwa serikali inakandamiza
uhuru wa kisiasa, uhuru wa kuongea na watu kukutana.
Bwana Ban amesema kuwa sio jambo zuri kwa polisi kuingilia maandamano ya upinzani.
Kwa upande wake afisaa mkuu wa maswala ya
kidiplomasia katika Tume ya Ulaya, Catherine Ashton, ametaka pande zote
za kisiasa kushauriana
Agizo hili linatokana na ghasia za kisiasa kati ya wanaharakati wa upinzani na polisi mapema mwezi huu.
Wiki jana mahakama nchini humo ilimchukulia
hatua kiongozi wa chama cha upinzani (Movement for Solidarity and
Development party) ambaye pia ni mwandishi habari wa zamani, Alexis
Sinduhije na wanaharakati wengine 71 kwa madai ya njama ya mapinduzi.
Hii ni baada ya maandamano yao salama ya Tarehe 8 mwezi huu kugeuka na kua vurugu kati ya wapinzani hao na polisi.
Huku hayo yakiarifiwa serikali ya Burundi
imechukua hatua ya kusitisha shughuli zote za chama cha upinzani cha MSD
kwa kipindi cha miezi minne baada ya kukishutumu kwa kuzua vurugu.
Chama hicho kimekanusha kusababisha vurugu zozote.