BREAKING NEWS

Monday, March 17, 2014

HIZI NDO AJIRA MPYA YA WALIMU WAPYA KWA AJILI YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWAKA 2013/14.







A: OFISI YA WAZIRI MKUU TAMISEMI INATANGAZA ORODHA YA WANACHUO WAHITIMU WA MAFUNZO YA UALIMU KAMA IFUATAVYO:-


i. Walimu wa Cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 17,928 


ii. Walimu wa Stashahada kwa ajili ya shule za sekondari 5,416 


iii. Walimu wa Shahada kwa ajili ya shule za sekondari 12,677 

 
Walimu hawa wamepangwa katika Halmashauri na shule za mazoezi za vyuo vya ualimu Tanzania Bara.
 
B: Kila Mwalimu (ajira mpya) atatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
  1. Kuripoti tarehe 01/04/2014 kwenye ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kupangiwa vituo vya kazi na kuanza kazi.
  2. Mwalimu atatakiwa kuwa na vyeti vyake halisi vya chuo na Sekondari 
  3. Walimu ambao ni waajiriwa wa Serikali waliokuwa wanajiendeleza kielimu wanatakiwa kurudi kwa waajiri wao ili kuendelea na kazi
  4. Fedha za kujikimu za siku saba (7) na nauli kwa walimu wapya zimetumwa katika Halmashauri walikopangwa walimu. Hivyo, kila mmoja aripoti katika Halmashauri aliyopangwa
  5. Mwalimu ambaye hataripoti ifikapo tarehe 10/04/2014 hatapokelewa tena na atakuwa amepoteza ajira yake.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates