Mwenyekiti wa TACINE Atanasi Kapunga akiongea katika mkutano huo |
Mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela Akiwa anafungua rasmi mkutano wa umoja wa majiji TACINE uliofanyika jiji Arusdha hivi leo |
washiriki wa mkutano mkuu wa TACINE wakiwa wanamsikiliza mgeni rasmi akiwa anafungua mkutano
Wito umetolewa kwa Halimashauri zote nchini kutafuta njia
mbadala za kuongezea Mapato yake ya ndani
tofauti na ilivyizoeleka kutegemea mapato yatokanayo na ushuru
mbalimbali wanaokusanya katika halimashauri zao.
Wito huo umetolewa jana
na mkuu wa ya wilaya ya Arusha John Mongela wakati akifungua mkutano mkuu wa asasi
ya umoja wa majiji Tanzania TACINE inaowakutanisha wakurugenzi pamoja na mameya wa majiji
tanzania uliofanyika mkoani hapa.
Alibainisha kuwa watendaji wa halimashauri zote hapa nchini wanatakiwa kuangalia namna
ya kuleta maendeleo katika halimshauri zao kwa kuunda miradi mikubwa yenye tija
ambayo inaweza kukuza mapato ya halmashauri zao.
Alisema kuwa inabidi halimashauri za majiji ziunde miradi ambayo itasiaidia kuongeza ushuru mkubwa wa
masoko wakati miradi hiyo kama ilivyo kuwa awali kwa halmashauri ya jiji la Arusha ilikuwa
ikikusanya kiasi cha shilingi milioni
kumi ambapo kiasi hicho kitasiaidia
kwani kitaongezaka adi kufikia milioni ishirini.
Mongela alisema kuwa Halmashauri
zina nafasi kubwa ya kufanya miradi mikubwa yenye tija na ambayo inaweza kuleta
faida kubwa na aendeleo makubwa.
Aidha aliwasihi wakurugenzi
pamoja na mameya wote kujitaidi kutumia ipasavyo nafasi zao za ungozi haswa
katika swala la kuwaletea wananchi maendeleo ili wakifikia katika kipindi cha kustaafu au kupunzika
katika nafasi zao za uongozi waache kitu hususa ni mradi ambao utakuwa wa kihistoria.
“iwapo meya au mkurugenzi
utafanya kitu ambacho kitakuwa kizuri
kama mradi ukifikia kipindi cha kustaafu au utakapo maliza kipindi chako mradi ambao uliufungua kipindi cha uongozi wako basi utanufaisha watu na
utapata sifa kubwa ambayo aita saulika”alisema Mongela
Kwa upande wa mwenyekiti wa TACINE ambaye ni meya wa jiji la mbeya Atanasi
Kapunga alisema kuwa dhamira kubwa ya umoja wao
kukutana katika jiji hili ni
kuwaakikisha majiji yote yana kuwa na hadhi ya
inayo fanana .
Aliongeza kuwa pia umoja huu unawezesha majiji haya kuwa katika hali ya madhari nzuri
pamoja na mpangilio uliomzuri ambao unahadhi ya jiji jambo ambalo litapelekea
kuongezeka kwa vipato na maendeleo kwa wananchi.
Kwa upande wa meya wa shinyanga
Gulamhafeez Mukadam alisema kuwa umoja huu umesaidia mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuleta maendeleo mbalimbali katika
halimashauri mbalimbali.
Alitolea mfano bara bara za
mijini ambazo zimejengwa katika halimashauri
mbalimbali alibainisha kuwa bila umoja huu wa majiji zisingewezwa
kujengwa.
Alibainisha kuwa changamoto moja
wapo wanaopata katika umoja huu ni pamoja na kukosa ushirikiano wa kutosha
kutoka katika wizara zetu jambo ambalo
alibainisha kuwa ni changamoto kubwa inayowakabili hivyo aliiomba wizara husika
ijitaidi kuwapa ushirikiano.
Pia Mukadam aliwasihi viongozi mbalimbali wa
halmashari za manispaa zote hapa nchini kuweka msimamo katika katika swala la
kuleta maendeleo na wasiangalie nyuma
walipotoka bali waangalie mbali wanapokwenda na kitu kana watawafanyia wananchi
nao wanufaike.