Ticker

6/recent/ticker-posts

MASHINDANO YA FOOSBALL @HEINEKEN KUJA KWA KASI

Heineken 1Unaambi wa michuano ya Foosball inalenga mashabiki wa mpira na watumiaji wa Heineken® waliopo Afrika Mashariki, na itakwenda sambamba na Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA) katika maeneo ya burudani 16.
• Heineken® ina mahusiano ya muda mrefu na Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), na itabaki kua mdhamini mkuu wa ligi hiyo hadi 2018
KAMPUNI ya Bia ya Heineken, imezindua msimu wa pili wa kampeni ya michuano ya Foosball kwa nchi za Afrika Mashariki, ambayo itaanza kufanyika hivi karibuni kwenye mikoa mbalimbali.

Heineken ambao pia ndio wadhamini wakuu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya (UEFA), imezindua mashindano hayo ambapo yatakua yakiendelea huku mashabiki wakifurahia kuangalia Ligi ya Mabingwa inayoendelea.
Akizingumza Dar es Salaam katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Heineken Tanzania, Uche Unigwe, alisema kuwa wameamua kuzindua mchezo huo baada ya mashabiki kuhamasika zaidi.
heineken 2Alisema kuwa michuano ya Foosball inafanyika kwa mara ya pili huku Tanzania kwa udhamini wa bia ya Heineken, baada ya kufanya vizuri mwaka jana.
Alisema kuwa michuano hiyo itaendana na mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya, inayoendelea ili kuweza kuwaweka mashabiki wa soka pamoja.
“Foosball ambayo inachezwa na mashabiki wengi Ulimwenguni, umekua kati ya michezo inayokua zaidi kila siku na hivyo tumeamua kuzindua tena kampeni hii ili kuendelea kuongeza mashabiki wa soka ” alisema.
Alisema kuwa kutokana na mafanikio makubwa waliyopata mwaka jana bia ya Heineken inayotambulika Kimataifa, wameamua kuboresha zaidi mchezo wa Foosball kwa ajili ya kuhakikisha wanafikia malengo.
“Kwa mwaka wa pili mfululizo Heineken inaendesha michuano ya Foosball, baada ya kufanya vizuri msimu uliopita, hivyo tunatarajia mashabiki wa soka wataongeza ufanisi zaidi kwenye msimu huu “alisema.

Post a Comment

0 Comments