BREAKING NEWS

Tuesday, March 4, 2014

RAIS KIKWETE AZURU VIKOSI VYA JWTZ VYA KOMANDO NA UHANDISI MEDANI MKOANI MOROGORO

Makomando wakimuonesha Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayuko pichani) mapigano bila shilaha wakati wa ziara yake.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia mapambano ya kareti, taikondo na judo yaliyokuwa yakioneshwa na makomando wa JWTZ (Hawamo pichani).
Komando wa JWTZ akionesha uwezo wa kukwepa mapigo ya risasi za adui kwa kupita juu ya mapigo hayo kwa kutumia kamba na kisha kuendelea na jukumu alilopewa.
Kamanda wa Kikosi cha Uhandisi wa Medani akitoa taarifa ya Utawala na Utendaji Kivita kwa (Hayupo pichani) mara baada ya Kikosi hicho kutembelewa.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifafanua maeneo kadha ambayo Wahandisi Medani wa JWTZ wamefanya kazi nzuri kurejesha miundombinu ya reli, barabara na madaraja hata pale ambako Mamlaka za Kiraia zimekuwa na maoni kuwa kazi hizo zingehitaji muda mwingi zaidi.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipewa maelezo kuhusu moja ya mitambo mipya inaotumiwa na Wahandisi medani kusafisha maji chumvi na baridi na kuwa maji safi na salama inayomilikiwa na Kikosi cha Uhandisi Medani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo kuhusu baadhi ya mitambo mipya ya kutengeneza barabara katika Kikosi cha Uhandisi Medani.
Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akivuka juu ya daraja jipya la medani lililojengwa kumuonesha uwezo wa Wahandisi Medani wa JWTZ kuendelea kusaidia usafirishaji wa zana na vifaa hata pale madaraja ya kudumu yanapoharibiwa kwa namna yoyote ile.
Picha/habari na Luteni Kanali Juma Nkangaa Sipe, Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Ulinzi na JKT 
 


Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Rais Jakaya Kikwete amefanya Ziara ya siku moja katika Vikosi vya Jeshi la Wanannchi wa Tanzania (JWTZ) vya Komando na Uhandisi Medali vilivyopo Mkoani Morogoro.

Akizungumza katika kikao maalum na Maafisa Askari wa vikosi hivyo,Rais Kikwete amesema ameridhishwa sana na utimamu wa vikosi hivyo kimafunzo na pia amehidi kukiongezea vifaa zaidi kikosi cha Uhandisi wa Medani ili kiweze kupambana na majanga hapa nchini.

Rais Kikwete pia amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kubuni mikakati ya kuondokana na Makazi ya muda.

Katika Kikao hicho,Rais Kikwete aliligusia swala ta tatizo la Maji linalovikabili vikosi hivyo,ambapo ameahidi kulishungulikia ndani ya kipindi hiki cha mwaka 2014.

Katika ziara hiyo,Rais aliambatana pia na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Wakuu wa Kamandi, Wakuu wa Matawi Makao Makuu ya Jeshi, Makamishna Wizarani na Wajumbe wa Mabaraza ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya na Mkoa wa Morogoro.
 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates