SOKOINE MEMORI MINI MARATHON KUFANYIKA APRIL 12 MONDULI

 

Gidabuday,W.F.
 
Tanzania inatimiza miaka 30 tangu kumpoteza kiongozi wake shupavu aliyefariki kwaajalimbaya ya gari Aprili 12 1984 mkoani Morogoro.

Si mwingine bali ni aliyekuwa Waziri Mkuu katika seriakali ya awamu ya kwanza, Hayati Edward Moringe Sokoine aliyezaliwa 1938 wilayani Monduli mkoani Arusha.

Tanzania itaadhimisha miaka 30 ya kifo cha Sokoine, ni kwa kukumbuka mema yote aliyoyafanya kiasi kwamba hadi leo anakumbukwa.

Tanzania pia mwaka huu inasherehekea maadhimisho ‘Jubilee’ ya miaka 50 tangu nchi zetu mbili za Tanganyika na Zanzibar ziungane.


Tanzania pia leo hii inaandaa historia nyingine tena ‘Katiba Mpya’ huu ni mwaka wa historia ambayo haipatikani kwingine Afrika kama si duniani.

Mimi kama mratibu wa mbio hizo ‘Race Director’ ninapenda kuwaomba wabunge wa bunge maalum la katiba watenge siku hiyo muhimu ya Sokoine Day kuja Monduli kusherehekea na watanzania wenzao ili wapate ile ‘Original Spirit’ waliyokuwa nao viongozi wetu.

Bilashaka watarudi Dodoma na Baraka za mzalendo halisi, Baraka ambazo zitawapa nguvu wabunge ili wawe na maridhiano katika maamuzi na hatima ya katiba mpya.

Kutakuwa nambioza Half Marathon yenye maana kamili ya “Mini Marathon” na pia kutakuwa na mbio za Kilomita 2 kwa wanafunzi pamoja na wakubwa maana philosophy ya michezo ni kwamba hakuna umri maalu! ‘Sports for All
 
Mwisho ninawatakia heri na safari njema kuelekea Monduli; “KUWA MZALENDOSAMBAZA UPENDO”.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post