Kweli
Urais hauna ubia wala muda ama sehemu ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali
popote ni sehemu ya kazi, kama inavyoonekana hapa ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka
Dar es salaam kuelekea Dodoma huku akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa
katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, Ijumaa, Machi 21, 2014.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia
Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la ya Kanuni za Bunge Maalum.