Zambia Olympic Youth Development Center |
Mwaka 2004 Tanzania ilipata bahati ya kuahidiwa kujengewa kituo kikubwa cha kisasa cha michezo (Tanzania Olympic Youth Development Center) ambayo ingegharimu USD 10million lakini viongozi wa TOC kwa kushirikiana na viongozi wasio wazalendo walikwamisha.
Kilichotakiwa
na IOC ni kuhakikishiwa kwamba eneo kubwa lisilo na utata wa kisheria
linapatikana ikiwa na vithibitisho vya kiumiliki ili hapo baadaye
kusiwepo na utata (contradiction) za kisheria.
Bila
aibu wala uzalendo kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) ilihakikisha
kwamba kituo hicho hakijengwi kwa sababu ya wao kuhofia masilahi yao ya
upatikanaji wa tenda za kimichezo katika center zao walizojiwekezea.
Kwa mfano: kama
mtu anapata tenda ya Copa Coca-Cola ya Tsh: Bilioni kila mwaka alafu
atawezaje kupata kiasi hicho cha pesa iwapo taifa litakuwa na center
yake? Hivyo kigogo mmoja tu mwenye center yake alishawishi kamati nzima
waikatae ofa hiyo ya IOC nao kwa akili zao ndogo wakaafiki upuuzi huo.
Hatimaye TOC ikashindwa kurudisha majibu kwa IOC ndipo IOC ikaamua kupeleka ofa hiyo Zambia na wazambia hawakuchezea nafasi hiyo na hivi sasa kuna kituo kinachoitwa Zambia Olympic Youth Development Center.
Je wizara na
baraza la michezo (BMT) wamefanya juhudi gani kuwachukulia hatua watu
hao? Watu ambao kimsingi ni ‘Wahujumu Uchumi’ maana kupindisha (Divert)
masilahi ya taifa ni kuhujumu uchumi wa taifa kwani watoto wengi wenye
vipaji wangenufaika na kituo hicho bila gharama.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia