Kituo cha Afya Tunduma
Kampuni
ya Bia Tanzania imetoa msada wa kisima cha maji kwa ajili kituo cha
Afya Tunduma chenye thamani ya shilingi milioni 24 chenye uwezo wa kutoa
lita 5000 kwa saa.
Afisa
uhusiano wa Kampuni hiyo Doris Malulu amesema kampuni ya Bia ni moja
kati ya Makampuni yanayoongoza kulipa kodi nchini na hivyo ina wajibu wa
kurudisha fadhila kwa Watanzania.
Malulu
amesema kampuni yake imetenga jumla ya shilingi milioni 450 kwa ajili
ya miradi mbalimbali ya maendeleo nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha
yenye nia ya kuisaidia serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Naye Afisa mipango Mji wa Tunduma Augustino Ngetwa amesema mradi huo utasaidia kumaliza tatizo la maji hivyo kuwa faraja kwa wagonjwa wanaotumia kituo hicho ikiwa ni pamoja na raia wa nchi jirani ya Zambia.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya mji wa Tunduma Aidan Mwanshiga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Momba Abiud Saideya amesema kuwa watahakikisha wanautunza mradi huo ili uwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho .
Aidha
Diwani wa kata ya Tunduma Frank Mwakajoka ameshukuru Kampuni hiyo kwa
kutoa mradi huo na hivyo kuwataka wahudumu kuitunza miundo mbinu ya maji.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji mdogo wa Tunduma Elias
Cheyo ameitaka kampuni ya bia kupanua wigo wa kusaidia Nyanja nyingine
kama vile elimu ili kufanya mji wa Tunduma kuwa na maendeleo zaidi.
|