Mwanamke: Je, unatafuta mchumba? Fuata kanuni hii hakika utapata mchumba mwenye tabia uzitakazo...
Kuna kitu kinaitwa nguvu ya mvuto, lakini pia huenda mmeshawahi kusikia au kusoma kitabu kinachoitwa “The Secret.” Ni
kitabu kizuri sana kinachoeleza kwa kirefu na kwa lugha nyepesi
inayoeleweka jinsi nguvu hii ya mvuto inavyofanya kazi. Katika kitabu
cha The Secret mwandishi
Rhonda Byrne anasema kwamba mawazo yetu ni kama sumaku. Kwa kawaida
sisi wanadamu tumezungukwa na nguvu ambazo hatuzioni lakini zipo kwa
hiyo Kwa jinsi tunavyofikiri hayo mawazo yanakuwa na nguvu ambazo
zinavuta kila kitu tunachowaza, kiwe kizuri au kibaya, ni lazima
kitarudi kilipotoka, ambapo sipengine bali kwako wewe mwenyewe.
Rhonda anazidi kubainisha utendaji wa mawazo yetu kwa kutoa mfano wa
ufanyaji kazi wa Luninga (TV). Kama wote tunavyofahamu kuwa ili kituo
cha kurusha matangazo ya Luninga kifanye kazi kunakuwa na minara
inayosafirisha mawimbi na kuyageuza katika mfumo wa picha na hivyo
kutuwezesha kuona matangazo ya luninga tukiwa majumbani kwetu. Wengi
wetu hatufahamu mitambo hiyo inafanya kazi namna gani, lakini tunafahamu
kwamba kila chaneli ina mawimbi yake ambapo kila tukichagua chaneli
fulani tunapata picha katika luninga zetu. Tunachagua mawimbi kwa
kubadilisha chaneli na ndipo tunapopata picha za matangazo kutoka katika
chaneli hiyo. Kama tunataka kuona picha na matangazo tofauti katika
luninga zetu tunabadilisha chaneli kwa kutafuta mawimbi ya chaneli
nyingine.
Sisi
kama wanaadamu tuko sawa na mnara wa kurusha matangazo ya luninga na
tuna nguvu kuliko minara ya kurusha matangazo iliyowahi kuwepo hapa
duniani. Mawimbi yetu ndiyo yanayoratibu maisha yetu na ndiyo
yanayoifanya dunia iwe kama livyo leo, kwani tunatengeneza mawimbi
kutokana na namna tunavyowaza. Ile picha tunayopata au tunayoiona
kupitia mawazo yetu, sio sawa na ile tunayoiona katika luninga zetu
sebuleni kwetu, bali ni picha ya maisha yetu! Mawazo yetu yanatengeneza
mawimbi na yanavuta kila tunachokiwaza na kuwa ndio maisha yetu halisi.
Iwapo tunataka kubadili chochote katika maisha yetu, basi inatulazimu
tubadili chaneli na mawimbi kwa kubadili namna yetu ya kufikiri.
Mwandishi huyo anaendelea kusema, kinachosabisha watu wengi wasipate
kile wanachokitaka maishani ni kwa sababu wanafikiria zaidi kuhusu kile
wasichokitaka badala ya kile wanachokitaka. Hebu tujaribu kuchunguza
mawazo yetu na kauli zetu, tutagundua siri kubwa. Kwani nguvu ya mawazo
ipo na inafanya kazi. Ugonjwa mkubwa sana unaowakabili wanadamu hapa
duniani karne kwa karne ni ugonjwa wa “sitaki” au “sipendi,” anabainisha mama huyo. “Watu
wameendelea kuacha ugonjwa huu uendelee kutawala katika mawazo yao,
vitendo vyao na kauli zao, wakiendelea kuzingatia yale wasiyoyataka au
wasiyoyapenda.” Anamalizia kusema mwandishi huyo.
Ugonjwa huo ndio unaowatesa baadhi ya wanawake wanaotafuta wapenzi. Mfano halisi ni kauli kama, “mimi sipendi wanaume wafupi,” au “mimi sipendi kuolewa na mwanaume mnyanyasaji….” na
kauli nyingine zinazofanana na hizo. Ukweli ni kwamba kitakacho watokea
wanawake wenye kutoa kauli kama hizo ni kuishia kuolewa na wanaume wa
aina hiyo….. kinachofanyiwa kazi na mawazo yetu ya kina (Unconscious Mind)
ni kile tunachokitamka, iwe ndicho tunachokitaka au tusichokitaka,
mawazo yetu ya kina hayajui neno sipendi au sitaki, hukuletea kile
ulichokitamka na kukijaza katika akili yako.
Kuna
wanawake wengi ambao wameolewa au wamewahi kujenga mahusiano na wanaume
ambao waliwahi kutamka hadharani kwamba kamwe hawatoweza kujenga
mahusiano nao au kuolewa nao. Hayo ni matokeo ya kauli zao ambazo
walizitamka bila kujua madhara yake. Kwa hiyo basi kwa kutumia kanuni
hiyo ya mvuto kama alivyosema mwandishi Rhonda Byrne mnatakiwa kuanza
kuratibu mawazo yenu na kauli zenu kwa kutamka aina ya wanaume ambao
mngependa kujenga mahusiano nao au kuolewa nao na haiishii hapo ni vyema
mkajiweka katika mazingira ambayo yatawavuta kuelekea mahali ambapo
mtakutana na aina ya wapenzi muwatakao. Huwezi tu kukaa nyumbani kwako
au kutembelea eneo moja hilo hilo kila siku halafu utarajie kukutana na
aina ya mpenzi umtakaye itakuwa ngumu, labda uwe na bahati sana.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia