Wahamiaji
Haramu hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika kata ya Ruaha
Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika doria ya kawaida
na kulitilia mashaka gari hilo lililokuwa limebeba matenga ya Nyanya.
Kiongozi
wa Wahamiaji Haramu,akiwagawia wenzake mikate ilionunuliwa na
wanahabari waliokuwepo kwenye tukio hilo kwa kushirikiana na Jeshi la
Polisi mkoani humo.
Kiongozi
wa Wahamiaji Haramu,akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na
sakata lao la kukamatwa nchini Tanzania,anasema wamesafiri nchini kwao
Ethiopia mpaka Tanzania kwa siku 21
Kamanda
wa
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akizungumza na
Waaandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye makao ya Polisi ya mkoani
humo,akithibisha kukamatwa
kwa wahamiaji haramu hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342
AJU likiwa
linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga wakitokea nchini
Ethiopia kuelekea nchini Afrika Kusini.
Roli lenye usajili wa namba T 342 AJU
likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga ndilo lililotumika kuwabeba wahamiaji hao.
Matenga ya Nyanya ambamo Wahamiaji hao walikuwa wamekaa.
Na Denis Mlowe,Iringa
JESHI la
Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 46 kutoka Ethiopia
waliokuwa wakielekea nchini Afrika ya Kusini.
Kamanda wa
Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amethibitisha kukamatwa
wahamiaji hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa
linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga..
Mungi
alisema wahamiaji hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika
kata ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika
doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo.
“Jeshi la
polisi lilipata habari za kiintelejensia kuwa kuna roli limebeba wahamiaji
haramu vijana wakajipanga na kufanikiwa kuwakamata wakiwa katikakati matenga ya
nyanya yaliyopangwa kwa pembeni na na kufanikiwa kuwakamata vijana hao 46
akiwemo mtoto wa miaka 17” alisema Mungi.
Alisema kuwa
dereva wa gari hilo anashikiriwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na
kusema baadhi ya Waethiopia hao 6 kati yao wana hati ya kusafiria (passport).
Katika hali
kuonyesha ukarimu kwa wageni hao haramu waandishi wa habari walioko katika
kampeni za jimbo la Kalenga wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa waliwapatia msaada
wa vyakula wahamiaji hao baada ya kuonyesha wanakabiliwa na njaa kali na kiu ya
maji.
Waandishi hao
wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa Iringa (IPC), Frank
Leonard walichangishana na kupatikana kiasi cha shilingi elfu 50 na kufanikiwa
kuwapatia vyakula hivyo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia